0
Chombo hicho kimepewa jina Kounotori
nakinaundiwa na kituo cha anga za juu
cha Tanegashima.
JAPAN:
Japan imezindua chombo cha anga za juu ambacho kitabeba mtambo maalum wa kukusanya takakata zilizopo anga za juu zikiizunguka sayari dunia.
Chombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700 ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo, nyaya hizo zitaundwa kwa madini ya aluminiamu na chuma cha pua, ambapo mtambo huo umeundwa kwa msaada kutoka kwenye kampuni moja ya uvuvi.
Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande milioni 100 vya taka kwenye mzingo wa dunia, inasemekana vipande hivi ni pamoja na vipande vya setilaini zilizoachwa kutumika, vifaa mbalimbali na vipande vya roketi.

Vingi ya vipande hivyo ni kati ya vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.

Vyombo vilivyorushwa kuzunguka
mzingo wa dunia, hizo ni taka kuizunguka dunia.
Takataka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kukwea kwenda anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957. Kugongana kwa satelaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya satelaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu.

Chombo hicho kilichopewa jina Kounotori (Korongo kwa Kijapani) na ambacho kimebebea mtambo huo, kilipaa kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Tanegashima, kaskazini mwa bahari ya Pasifiki Ijumaa kuelekea kituo cha kimataifa cha anga za juu.

Watafiti wanasema nyaya hizo zinazotumia nguvu za maalum za sumaku ambazo kwa Kiingereza huitwa electro-dynamic, kitazalisha nguzu za kutosha kubadili mwelekeo wa vipande hivyo na kuvielekeza kwenye anga ya dunia ambapo vitateketea.
Kampuni ya wataalamu wa kuunda nyavu za kutumiwa na wavuvi Nitto Seimo Co, ambayo imekuwepo kwa miaka 106, imeshirikiana na shirika la anga za juu la Japan kuunda mtambo huo.  Majaribio ya kutumia mtambo huo ni moja ya juhudi za kuhakikisha anga za juu ni salama kwa wana anga kwa kupunguza taka.
Inatarajiwa kwamba itasaidia kulinga vituo vilivyo anga za juu pamoja na setilaiti za kutabiri hali ya hewa na zile zinazotumiwa kwa mawasiliano, vyote vya thamani ya mabilioni ya dola.
Wataalamu wanasema kuna manufaa mengi yatakayotokana na kuondolewa kwa taka kwa kutumia mradi huo wa Japan, lakini wanasema huenda ukafanikiwa kwa vipande vikubwa pekee vya taka.





Habari hi ni kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.

Post a Comment

 
Top