0
Profile Photo: Mbunge Lema mwenye gwanda jeusi akiongozwa na askari wa jeshi la magereza huku wananchi wakishuhudia.
Profile Photo: Godbless Lema akipanda kwenye Landrover ya Polisi kutokea kituo cha polisi mjini Arusha.


ARUSHA.
Mbunge Arusha mjini kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Godbless Lema akiwa anaendelea kukaa na kupata madhira kwa kukaa lupango, huku ikionekana hata mwaka mpya ataushuhudia akiwa huko mawakili wake wamelalamika kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha hoja yao mahakama kuu kanda ya Arusha.
Peter Kibatala amabaye ni mmoja kati ya mawakili wanaomtetea mbunge huyo amesema kuwa upande wa serikali badala yake umepeleka notisi mahakama kuu ya kukata rufaa ili kuendelea kuchelewesha utaratibu wa Lema kupewa dhamana. "Tayari upande wa mashtaka wameshaona kwamba Mahakama kuu inaelekea kusikiliza hoja ya ziada ambayo upande wetu ni kuwa mteja wetu kunyimwa dhamana na mahakama ya chini," alisema kibatala.
Wakili Kibatala ameendelea kusema kuwa kama inavyojulikana mahakama ya rufani huwa haikutani kwa haraka na wakati mwingine inachukua miezi minne, sita hama mwaka mzima, kitu ambacho kitamuacha mteja wetu akae jela kwa muda huo wote na kuwa kesi ambayo awali ilipangwa Januari 2 hivi sasa haitakuwepo na hivyo wanasubiri uamuzi wa mahakama kuu utakaotolewa Januari 4 mwaka ujao 2017.
Mbunge huyo anashtakiwa kwa kutumia lugha ya kuchochea inayoweza kusababisha hali ya sintofahamu inakumbukwa mnano Novemba 11, hakimu mkazi alimpa Lema dhamana lakini kabla ya kutoa masharti ya dhamana hiyo, upande wa serikali ulitoa notisi ya kukata rufaa, hata hivyo Kibatala alisema upande wa utetezi tayari wameshawasilisha hoja zao Ijumaa kama walivyotakiwa na mahakama kuu.
Katika hati ya maandishi yenye kuelezea hoja za upande wa Lema inaeleza kuwa wamesikitishwa na kitendo cha serikali kutowasilisha hoja yao kuhusu ombi la kunyimwa dhamana kwa mteja wao waraka huo umeendelea kueleza kuwa kitendo cha upande wa serikali kutowasilisha hoja yao ya maandishi ni sawa na kutofika mahakamani, na hivyo ni wazi kwamba linapelekea rufaa kutupiliwa mbali.
Mawakili wa mbunge huyo Jumatano iliyopita walikubali rufaa ya serikali kuanza kusikilizwa kwa njia ya maandishi, "Tumeona kuwa matokeo ya rufaa ni moja, rufaa ya Lema isimamishwe mpaka pale rufaa ya serikali itakapowasilishwa katika mahakama kuu," alisema Bw. Kibatala.
Jaji wa mahakama kuu alitoa nafasi kwa pande zote mbili kuwasilisha hoja za ziada, na kuwa wao wataendelea kusimama pale pale kwamba wanapinga uamuzi wa mahakama hiyo ya chini kumnyima mteja wao dhamana.


Source: VOA

Post a Comment

 
Top