T.News Photo Profile:
Maxence Melo
alipokuwa akitoa
mada katika
mkutano wa chama cha wenye
Blogs nchini
hivi karibuni jijini Dar Es Salaam.
|
DAR ES
SALAAM.
Mkurugenzi na
Mwazilishi wa Mtandao wa kijamii nchini Jamii Forums Maxence Melo anaendelea
kushikiliwa na Jeshi la polisi katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam kwa
siku ya nne sasa. Wakili wa Melo Benedict Ishamakaki amesema hadi Jumatano
jioni alikua bado yuko katika mikono ya polisi kwa tuhuma kwamba amezuia
uchunguzi wa polisi kwa kuwanyima taarifa muhimu.
Benedict alisema “Lakini hakuna kosa linalomnyima dhamana
kwani ni makosa yale yale yaliyokuwa yanamkabili siku za nyuma ambayo tulikuwa
tumeyaombea ufafanuzi kutoka mahakama kuu.”
Alisisitiza kuwa katika barua za
awali ambazo jeshi la polisi lilimuandikia Melo kumtaka atoe taarifa zinazohusiana
na wanachama wake, lakini wakili huyo alieleza kuwa sheria ya mtandao imeeleza
habari feki kama ni kosa la jinai, akihoji kwamba ni nani ambaye anaamua kwamba
hili ni la kweli au hili ni uongo katika mazingira hayo.
Kwa mujibu waBenedict ziko taarifa
zilitolewa na watoboa siri kuhusu makampuni binafsi ambazo zinazituhumu kampuni
hizo kwa ukwepaji kodi na vitendo vya ufisadi. Benedict anasema; “Tunasikitishwa
kutokana na kuzungushwa kwa mteja wetu na kupigwa dana dana kuhusu dhamana
yake, ambapo leo tayari imefikia siku ya tatu.” hata hivyo
alimalizia kwa kusema sera za jamii forum ziko wazi tangu ilipoanzishwa mwaka
2008, kama ingekuwa inahatarisha usalama wa taifa ingekuwa imefungwa zamani.
Inaelezwa kuwa Teknolojia wanayoitumia
Jamii Forums ya kuficha taarifa (encryption) katika kumsajili mtumiaji wa mtandao
huo haiwawezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda kama yeye mwenyewe atakubali
kwa hiari yake kujiweka wazi mtandaoni.
Post a Comment