0
Upande wa kushoto wa gari hilo ukiwa unaungua kwa kasi kutokana na itilafu ambazo shuhuda wa ajali hiyo hakuweza kuelewa kilichotokea.
Dereva wa lori hilo mwenye shati nyeupe akijaribu kuvuta Kamba ili kuvuta turubai iliyokuwa imefunika shehena ya mzigo uliopo kwenye tela la nyuma, pembeni yake ni msaidizi wake (utingo).
Mmoja wa wafanyakazi wa roli hilo ambaye alijitolea mhanga kujaribu kuokoa baadhi ya mali zilizopo kwenye tela la nyuma akijaribu kuondoa turubai juu kabisa huku moto ukiwa unaelekea eneo hilo.
Sehemu ya moto unaoteketeza roli hilo lenye namba za usajili T 696 DOQ



SINGIDA:
Lori aina ya scania lililokuwa linatokea jijini Dar Es Salaam likielekea mikoa ya kanda ya ziwa limeshika moto kutokana na sababu ambazo dereva wa gari hilo ameshindwa kuelezea kutokana na hali ya moto iliyokuwa ikiendelea eneo la tukio.


Gari hilo lenye namba za usajili T 898 DCQ lililokuwa limesheheni mzigo wa viti na meza za plastiki lilianza kushika moto kutokea eneo la injini kisha kushika eneo lote la kichwa cha gari na kuwaka mpaka sehemu ya mizigo kwa nyuma.


Ajali hiyo imetokea mkoani Singida katika eneo la sukamela ukitokea Dodoma ni takribani saa moja na nusu kwa mwendo wa kawaida wa gari, ambapo kijana mmoja aliyejulikana kwa jina Abdalah Sadiq ambaye alikuwa abilia kwenye roli hilo anasema, “…tulikuwa kwenye mwendo wa kawaida tu gafla tukashangaa moto ukitokea kwa chini ndipo dereva akasimamisha gari


Post a Comment

 
Top