Watu
wakiwa wamerejea katika kazini ili kuendelea kuwajibika kutoka katika mapumziko
ya krismasi, huku wakijipanga kukaribisha mwaka mpya, baadhi ya raia katika nchi
za ughaibuni, sikukuu hiyo imewaacha katika majonzi makubwa baada ya kupatwa na
dhoruba ya kuondokewa na ndugu zao.
 |
.Moja ya
eneo ambalo lilikumbwa na shambulizi katika mji wa Chicago nchini marekani
likiwa chini ya uangalizi wa polisi
|
 |
Maofisa usalama wakiondoa mwili wa raia
aliyejeruhia katika eneo la shambulizi.
HABARI KWA UNDANI:
MAREKANI.
Watu wapatao 11wameuwawa na wengine 37 wamejeruhiwa wakati wa maadhimisho ya Krismasi mwishoni mwa wiki iliyoisha, asubuhi mapema siku ya krismasi pekee watu watano waliuawa na mwingine 11 walijeruhiwa, taarifa ya polisi katika mji wa chikago lilipotokea shambulio hilo walisema.
Idadi hiyo ya watu waliouawa imefanya jumla ya watu
waliouawa kwa risasi katika kipindi cha mwaka 2016 kufikia 750, na kufanya mji huo wa chicago kuongoza kwa mauaji katika kipindi cha miongo miwili.
Matukio kama haya yamekuwa yakitukio sehemu
kadhaa na wauaji wakitokomea kusikojulikana, Polisi nchini humo wamesema
pia kwamba watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyohusisha
bunduki, na kuyahusisha na magenge ya uhalifu.
Kutokana na tukio hilo hakuna mtu alikuyekamatwa kwa
shambulizi hilo. Pia mwishoni mwa wiki, watu watatu waliuawa na wengine tisa
walijeruhiwa kati ya Jumamosi na mapema Jumapili, na watu wengine watatu waliuawa
na 17 walijeruhiwa siku ya Ijumaa na asubuhi ya Jumamosi ya sikukuu.
|
Post a Comment