Moja ya gari
lilioundwa na chuo hicho na ambalo limekuwa likitumika na kutoa mafunzo kwa
vitendo kuanzia makenika mpaka mafunzo ya kuendesha, linajulikana chuoni hapo
kwa jina maarufu kakakuona.
|
Wanachuo wa Bruno
Vocation Training Centre wakiingia kwa ajili ya kuanza sherehe za kuhitimu
mafunzo yao.
|
Kutoka kushoto
ni mkuu wa chuo cha BTVC Otmara Mwakyusa,
mjumbe wa serikali ya mtaa Enock Saiman, Mgeni rasmi Barua Mwakilanga na
Mkurugenzi wa Shule Bruno ndege.
|
Ndugu jamaa na
marafiki ambao wamefika chuoni hapo BVTC kwa ajili ya kushuhudia kuhimu kwa
vijana wao na kukabidhiawa vyeti vya kuhitimu mafunzo.
|
Mafunzo kwa
vitendo mkuu na mmiliki wa chuo Bruno Ndege akitoa maelezo yahusuyo injini ya
gari (mfano) ya mafunzo iliyopo chuoni kwa mgeni rasmi.
|
Mkuu wa chuo Otmara Mwakyusa BVTC akisoma risala kwa
mgeni, wahitimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika
chuo hicho Buguruni Jijini Dar.
|
HABARI KWA UNDANI:
DAR ES SALAAM:
Chuo cha mafunzo ya ufundi na makenika kilichopo Buguruni
jijini Dar Es Salaam Bruno Vocation Training Centre kimefanya mahafari yake ya
ishirini pamoja na sherehe za kutimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake kwa
wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ufundi ikiwa ni jitihada za kuwawezesha vijana
kupata elimu ya ziada waweze kujitegemea.
Akiongea wakati wa sherehe za mahafari hayo
mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni Mivinjeni ambaye ni mgeni rasmi amesema tangu wakati wa
utawala wa Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere aliona umuhimu wa
kuaznisha vyuo vya ufundi kwa kanda hapa nchini ili kuweza kuwafanya watanzania
kuwa na uzoefu binafsi kwa ajili ya maendeleo ya taifa hususani kwa viwanda vya
hapa nchini.
Mkuu wa chuo hicho Otmara Mwakyusa amebainisha mafanikio kadhaa
waliyopata kutokana na kutoa elimu ya ufundi kwa vitendo na nadharia ambapo
baadhi wa wahitimu wameweza kupata ajira katika makampuni kadhaa hapa nchini
pamoja na wengine kujiajili kutokana na uwezo waliopata kutoka chuoni hapo.
Post a Comment