Benjamin Mkapa akiongea na wanahabari.
|
BURUNDI:
Wanasiasa
wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa
rais wa Tanzania za kutatua mzozo uliopo nchini humo.
Hii inatokana baada ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si
jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.
Inakumbukwa nchi ya Buurndi
ilitumbukia kwenye mzozo mkubwa wa kisiasa baada ya Rais Nkurunziza kutangaza
kuwa angewania muhula wa tatu wa kiti cha uras nchini humo, ambapo mamia ya
watu waliuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.
Rais mstaafu Mkapa akiwasili nchini Burundi.
|
Rais huyo mstaafu alipewa jukumu la
kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yatafikiwa mara ifikapo
mwezi Juni mwaka ujao wa 2017.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani
walio uhamishoni wanatafutwa na serikali ya Burundi kwa kupanga maandamano ya
kupinga hatua ya Rais Nkurunziza ambapo serikali yake imezitaja kuwa za kihalifu
na wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli
mwezi Mei.
Post a Comment