SONGEA:
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) kufa baada
ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi,
kijana huyo alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma
(Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo
nyoka wake huyo.
Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba
aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake
hilo halikusikilizwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya
Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724
AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.
 |
Profile photo.
Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika
katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa
pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo
alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha
kichwa.
Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo
aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake
alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.
Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za
kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo
la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi
kumfanya apige kelele.
Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya
jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo
hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza
maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na
kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.
Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba
ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini
huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani, habari zinasema kuwa,baada ya Komba
kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo
juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake
zilishindikana kwani Komba alifariki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,
Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa
marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi
maiti katika hospitali ya rufaa Songea.
Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi
amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea
ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye
kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye
anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Ruvuma.
Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa
wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea
madhara kama vile majeraha au vifo.
|
Post a Comment