Profile photo: Mwanga unawake kwenye giza na kuleta
nuru.
|
DAR ES SALAAM.
Kupanda kwa garama ya maisha kuna njia
nyingi zinazosababisha ikiwemo vyakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi
na yasiyo ya msingi.
Kwa mazingira ya kawaida ubo mahitaji
muhimu kama umeme kwa maendeleo ya taifa lolote lazima kuwepo nauboleshaji wa
baadhi ya vitu muhimu, shirika la umeme nchini Tanesco liliomba kupandisha
garama za umeme toka mwezi wa Oktoba 4.2016, kwa asilimia 18.19% kuanzia tarehe
01.01.2017.
Ambapo katika pendekezo hilo linalenga
kuongeza bei ya sasa ya umeme kutoka shs 242.2 kwa unit mpaka shs 286.28 kwa
unit, ambapo pendekezo hili linaonyesha mgawanyiko kwa uzalishaji wa umeme shs
155.35unit kusafirisha shs 23.76unit na kusambaza shs 107.17unit, hata hivyo pamoja
na kuwepo kwa ushauri kutoka mabaraza ya watumiaji kutoa ushauri kwa Tanesco
kuacha kupandisha garama, ushauri huo umefanyiwa kazi katika hatua kadhaa.
Baadhi ya watumiaji wa nishati hiyo kupitia balaza
la ushauri la seriakali -GCC, balaza
la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA
–EWURA CCC, Shirika la umeme la Zanzibar –ZECO, Mamlaka ya maji singida, Kiwanda
cha saruji cha Simba na wananchi kwa ujumla, walitoa mapendekezo yao kupinga
kuongeza garama hizo kutokana na muda mfupi tu umepita ambapo waliomba
kupunguza garama za umeme.
Pamoja na uchambuzi
wa kina EWURA imejiridhisha
kuwa bei inayopendekezwa na TANESCO
kwa mwaka 2017 ni ya juu kama inavyoelezwa lakini kutokana na kutambua garama
za haki tuzinazoingiwa na TANESCO
ndiyo zinazingatiwa, hivyo gharama za uendeshaji zilipunguzwa kutoka zile
zilizoombwa na TANESCO
shs 286.23 na kurudi kufikia shs 263.02 kwa unit.
Vilevile mgawanyo mpya wa watumiaji wa watumiaji wa
nishati hiyo utakuwa katika makundi tofauti, kuna D1 hawa ni watumiji wadogo
wanaotumia umeme chini ya 75unit, T1a wateja wa kawaida ambao ni wa majumbani, biashara
na taa za barabarani lakini pia kuna T1b –Viwanda vidogo nk, kutokana na
mgawanyo huo garama zitaongezeka kulingana na mtumiaji kwa kundi alilopo.
Post a Comment