0
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiongea wakati wa hafla ya kutiliana sahihi za kuanza kwa mradi wa uboreshwaji wa barabara na miundombini jijini Dar Es Salaam.
Mwakilishi wa kampuni ya China Railway 7th Construction wa kulia akibadilisha dodoso za mradi na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kushoto mara baada ya kuweka sahihi za kuanza kwa mradi.
Baadhi ya wawakilishi kutoka serikalini, mstahiki meya  Chales Kuyeko mwenye miwani , Mkuu wa wilaya Sophia mjema mwenye gauni jekundu, mwakilishi wa kampuni iliyopewa kazi ya ujenzi wa miundombinu ya CR7C aliyenyanyua dodoso wakiwa katika picha ya pamioja mara baada ya kutiliana saini mkataba. 


DAR ES SALAAM.

Mradi mkubwa wa uboleshaji wa miundominu katika manispaa ya wilaya ya Ilala utakaofanyika kwa awamu kadhaa na unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unatarajiwa kuanza kutekelezwa mara baada ya kusainiwa kwa utekelezaji wake leo katika ukumbi wa Anatouglo mnazi mmoja jijini Dar Es Salaam.

Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka mmoja unahusu barabara zisizo za lami na utaanza kwa hatua ya uboreshajina  ujenzi wa miundombinu ya madaraja na barabara za mitaani zinazounganisha mitaa kama ile ya Olimpio yenye urefu wa 0.2km iliyopo upanga, baadaye kurekebisha na kuweka mitaro na baadaye kurekebisha mitaa kupitia hatua kadhaa zilizopo tayari.

Wakati wa kusaini mkataba huo, mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya ilala Msongela Nitu na mstahiki meya Charles Kuyeko kusimamia kikamilifua mradi huo uwe wa viwango vya hali ya juu na usije kuwa wa kurudiarudia.


Utiaji sahihi umefanyika kati ya halmashauri hiyo na kampuni iliyopewa ukandarasi  ya China Railway Seventh Group mbele ya viongozi kadhaa wa serikali na wawakilishi wa benki dunia pamoja na mstahiki meya na viongozi wengine.

DC Mjema amefafanua kuwa mradi huo wa DMDP utapendezesha mitaa na kuondoa foleni jambo ambalo litawasaidia wananchi wa maeneo husika kupunguza muda wa kwenda katika shuguli zao, hivyo amewahimiza mkurugenzi na mstahiki Meya wa ilala kuhakikisha kuwa barabara na madaraja yanajengwa kwa viwango na kwa wakati kama ilivyopangwa.

DC Mjema ameeleza kuwa mradi huo utazipitia barabara za Ndanda, Olympio, Kiungani, Omary Londo na Mbarouk ambazo zote zitakuwa na urefu wa kilomita 2.8 kwa kila moja, ambapo katika hatua nyingine DC Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha maroli yaliyozidi kiwango cha kubeba mizigo hayapiti kwenye miundombinu hiyo kwani yataleta uharibifu.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Charles Kuyeko ameeleza kuwa watajitahidi kuusimamia kikamilifu mradi huo wa DMDP ambapo zaidi ya bilioni 11.1 zimetengwa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi huo, huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Msongela Nitu akihaidi kuyafanyia kazi maagizo yote ya Mkuu wa Wilaya.




Post a Comment

 
Top