0
Naibu waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mh. Edwin Ngonyani 
Naibu waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mh. Edwin Ngonyani amewaasa watendaji wa wizara hiyo kuzingatia nidhamu ili kuleta tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi pamoja na kuwahusia kuwa ikiwa mtumishi atakosa nidhamu ni wazi anazorotesha ufanisi sehemu ya kazi, maana nidhamu ni kiungo muhumu katika kupata mafanikio.


“uwepo wa migogoro baina ya watumishi sio tu ni ukosefu wa nidhamu bali pia ni kikwazo kikubwa katika kuleta ufanisi mahali pa kazi…” amesema Naibu Waziri, Edwin Ngonyani.

Hata hivyo ametoa rai kwa vingozi kufanya kazi kwa uwazi kwa kuthamini michango ya wanao waongoza na amesisitiza kuwa haipendezi kuona mambo yanayoendelea sehemu ya kazi ilihali watumishi wenyewe hawajui kinachoendelea “tuache tabia za ubwana bali tuongoze walio chini yetu kistaarabu kwa uadilifu mkubwa na kwa ridhaa yao, tukifanya hivyo tutapunguza kama sio kuondoa manung’uniko na migogoro katika sehemu zetu za kazi” Alisema.

Kwa upande mwingine ametoa amegusia mjadala utakaohusu mambo kadhaa kama; kupitia na kupitisha miundo ya watumishi na mgawanyo wa kazi, taarifa za saccos –taa na uzinduzi wa katiba ya chama cha kufarijiana pamoja na taarifa za utendaji ambapo kupitia mijadala hiyo italeta suluhisho la changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo yao.

Post a Comment

 
Top