Kiwango cha homoni huongezeka
kwa kiwango kikubwa pale mwanamke
anapokuwa na
mimba.
|
Wanasema uja uzito hupunguza seli za ubongo kwenye
baadhi ya sehemu za ubongo wa mwanamke, ili kumuwezesha kuhusiana vema zaidi na
mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama.
Uchunguzi ulifanywa kwa wanawake wapatao 25 waliokuwa
wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo kudumu
kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za
ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo,
lakini hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka
kumbukumbu ambapo wanawake wengi husema huwa wanajihisi kuwa wasahaulivu na
kuwa wepesi wa kuekwa na hisia wakati wanabeba mimba.
Mabadiriko hayo kwenye ubongo
yanaaminika kuwaandaa wanawake
kuwa na uhusiano mwema
na watoto wao.
|
Watafiti
kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leiden walichunguza
ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na
miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo.
Walilinganisha mabadiliko hayo kwenye
ubongo wa wanawake na ubongo wa wanaume 19 waliokuwa ‘baba’ kwa mara ya kwanza,
wanaume 17 ambao hawakuwa na watoto na wanawake 20 ambao hawajawahi kujaliwa kupata
watoto, walishuhudia kupungua sana kwa seli za ubongo katika maeneo ambayo
hutumiwa na ubongo kuhusiana na watu wengine.
Wanasema mabadiliko hayo huenda ni ya
kuwafaa wanawake kwa njia kadhaa zikiwemo kuwawezesha kupangia mahitaji ya
watoto wao, kuwa na ufahamu zaidi kuhusu hatari kwa watoto wao kutoka kwa jamii
na pia kuwawezesha kuwa na mahusiano zaidi na watoto wao.
Source BBC NEWS
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.