Bumija
Mvungi –ARUSHA.
Majukumu ya wanawake
yanafanana wakiwa nyumbani ni wasimamizi wa familia,wakiwa ofisini ni watenda
kazi na wakiwa sehemu za biashara ni wafanya biashara hivyo ndio maana taasisi
ya TAGLA chini ya usimamizi wa ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora ilianza
kutoa mafunzo ya kumjengea uwezo mwanamke, kujiamini sehemu ya kazi toka mwaka
2011.
Akizungumza na wandishi
wa Habari mkurugenzi mtendaji wa TAGLA ndugu Charles Senkondo
amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kumuwezesha mwanamke kuwa kiongozi
bora kwa kuzitambua furasa zilizopo akiwa Ofisini, nyumbani na kwenye biashara
kwa kuzingatia namna ya kuweza kumiliki fedha sehemu za kazi pia kuwa na
maamuzi ya utekelezajia wa furusa hizo.
Mafunzo hayo yamelenga
mikoa yote hapa nchini kwa Taasisi za Umma, Taasisi zisizo za Umma kwa wafanyakazi,
wajasiriamali na vijana wa elimu ya juuu [Wanawake] kwa lengo la kumwezesha
mwanamke kuwa kiongozi bora kwa kuwapatia Elimu katika nyazifa mbali mbali
Serikalini.
Aidha kwa upande
wa washiriki katika mafunzo hayo Bi Hilda Tegwa ambaye ni Meneja Rasilimali
watu Mamlaka ya Mapato Tanzania alisema kuwa mbinu walizojifunza ni za Uongozi
usimamizi na namna ya kuandaa majukumu ya kazi hivyo Elimu
waliyopata wataifikisha kwa wanawake wa Vijijini ili waweze kuzitambua
fulsa walizonazo Serikalini, majumbani na kwenye biashara wanazozisimamia na
jamii kwa ujumla.
Naye Mwalimu Flaria
Faraja ambaye ni Mkurugenzi Chuo cha kulelea Watoto yatima Tanzania amesema
kwamba wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni fedha, elimu haijawafikia
wengi na waniomba TAGLA itoe semina kwa wanawake wabunge ili waweze
kusikia kilio chao na mikakati waliyojiwekea ili kuwawezesha hata wanawake
wajasiriamali kushiriki katika mafunzo hayo na ameiomba Serikali ione umuhimu na ifanye
utaratibu wa kuwawezesha fedha ili kuweza kuwafikia watu wengi Zaidi.
Post a Comment