Mh.
Philip Mpango (wa pili kuli) akikata utepe kwenye kibao maalum
kinachotambulisha ufunguzi rasmi wa kituo hicho cha elimu ya uhasibu kilichopo
nje kidogo ya jiji la Dar.
|
Jiwe la Ufunguzi wa kituo.
|
Waziri
Mpango, watatu kushoto akiangalia moja ya ukumbi uliopo katika katuo cha
mikutano na taaluma ya uhasibu, ukumbi huo unan uwezo wa kuchukua watu 80.
|
Lango
kuu la kuingilia katika kituo cha mikutano na taaluma ya uhasibu kilichopo nje
kidogo ya jiji la Dar Es Salaam katika eneo la Bunju A.
|
Kwa
nje ukiwa unatoka sehemu ya kuegeshea magari unaonana na muonekano huu kwa
upande wa kaskazini ukiwa unaingia kupitia lango kuu.
|
Ukiingia
geti kuu upande wa kushoto kuelekea vilipo vyumba ukiwa unatembea na kugeuka
gafla macho yataonana na mazingira haya ukiangalia mlango wa kuingia ukumbi mkubwa.
|
Wakati
mwingine kuogelea kwenye maji chumvi baharini unakuwa na hofu au kuogopa kunakotokana
na kukosa uzoefu wa maji chimvi, hapa kwenye kituo wamekuwekea bwawa la
kuogelea lenye kina tofauti.
|
Kwa
mbali ni majengo ya vyumba vya hotel ambavyo vinafikia 108 ambavyo ukiwa ndani
unatizamana na bahari ya hindi kama hipo karibu nawe.
|
Hii
ni sehemu ya kuingilia kwenye kumbi za mikutano, hapa ni moja ya njia kuelekea
kwenye ngazi ndipo uingie ndani, kama kwenye mwamba lakini ni ubunifu wa
watanzania wazalendo
|
Hapo
ni sehemu ndogo tu ya ukumbi huu mkubwa unaochukua watu zaidi ya 900 kwa mara
moja wote wakiwa wamekaa na kufuatilia tukio lililowafanya kuwepo ndani hapo.
|
Hizi
zinazoonekana ni sehemu ya kurushia picha, sinema au kufundishia zimewekwa mbili
kubwa mtu yeyote hashindi kufuatilia tukio kwa kutumia screen hizo.
|
Wahasibu
na wanataaluma wakiwa wameketi ndani ya ukumbi huo wenye kila aina ya huduma. Kwenye
vioo kwa juu ni sehemu wanapokaa waongozaji wanaoweka sawa vipaza sauti na
mambo ya usalama.
|
Post a Comment