Waziri
wa fedha na mipango Mh Philip Mpango kulia akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili na kulia kwake anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi mkuu wa
NBAA Pius Maneno.
|
Wakiwa
tayari kufungua mkutano mkuu wa mwaka kushoto ni mkurugenzi mkuu wa NBAA Pius
Maneno waziri Mpango (katiakati) na Mwenyekiti wa bodi GEPF Joyce Shaidi.
|
Mkurugenzi
Mkuu wa NBAA Pius Maneno akitoa maelezo ya mwanzo kuhusu uwekezaji huo mkubwa
wakati wa kuanza rasmi shuguli ya uzunduzi na kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa
wahasibu.
|
Wahasibu
na wataalam wa mahesabu wakipiga makofi kupongeza hotuba yam h waziri mara
baada ya kumaliza hotuba.
|
HABARI KWA UNDANI:
Uzinduzi wa kituo cha kisasa cha mikutano chenye
hadhi ya kimataifa kilichoko nje kidogo ya jiji katika eneo la Bunju,
umefanyika huku waziri mkuu Kassim Majaliwa akitarajiwa kufungua kituo hicho
kilicho na majengo ya hotel kama yanavyoonekana pichani.
Mkurugenzi mtendaji wa NBAA Pius Maneno anasema
sheria ya mashirika ya umma ya mwaka 1973 iliyofanyiwa marekebisho 1995 ndiyo
iliyopelekea kuwepo kwa kituo hicho chenye ukubwa wa heka 59654, ambapo ujenzi
wake ulitarajiwa kutumia shs 14bilioni lakini kutoka na kuchelewa kukamilika
umetumia shs 33 bilioni, katika hatua nyingine unalenga kupunguza garama kutokana
na ukodishaji wa kumbi za mikutano, vyumba kwa garama ndogo na katika eneo hilo
kuna.
Moja wa kumbi katika kituo hicho una uwezo wa
kuchukua watu 900 kwa mara moja huku kumbi nyingine zikiweza kuchukua mpaka
watu 600, ambapo kuna vyumba vya kulala 108 vinavyotoa huduma ndani kwa ndani (self-container)
na viwanja vya michezo nk.
Kituo hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya GEPF na
APC, pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa kama uchelewaji kwenye kuanza kazi,
ukosefu wa maji ya uhakika, kituo hicho kilichobuniwa na wataalam wazalendo,
kinatarajiwa kutoa huduma kwa watazania wote.
Naye mwenyekiti wa NBAA Isaya Jairo ameshukuru
serikali kupitia taasisi zake kuweza kutoa fedha na kushiriki katika kuwekeza
kwa fedha nyingi katika eneo hilo, huku akiona haja ya utaalamu na ushauri
kutoka serikali una nafasi muda na wakati wote, pia alibainisha changamoto
kadhaa kwa nbaa kukosa wafanyakazi wanaojitosheleza akitoa mfano uhitaji wa
wafanyakazi 75 lakini kwa sasa wana wafanyakazi 52 ikiwa ni pungufu.
Akizungumza mara baada ya uzindua kwenye jiwe la
msingi la kituo hicho pamoja na mkutano wa mwaka wa wahasibu, kwa niaba ya
waziri mkuu, waziri wa fedha na mipango Philip Mpango amebainisha mambo kadhaa
ambayo yanapaswa kufanywa ili kukiwezesha kituo hicho kufikia malengo ambayo
GEPF na mshirika wake katika kituo hicho APC wanatarajia kupata.
Akigusia taaluma ya uhasibu ambayo serikali inaitambua
kwa maana ndiyo inahusika katika kuangalia na kutunza fedha, amesema “taifa linaona matunda yake kupitia wahasibu waliopo
katika sekta mbalimbali za serikali na watu binafsi,pamoja na kuwa bado ni
wachache, tunajivunia kwa hao japo CPA inabidi ijitathini kuongeza wigo.”
Waziri mpango amekwenda mbali kwa kusema, baadhi ya
wahasibu wanatumia nafasi zao kuwaibia watanzania kwa kutumia kalamu na komputa,
“hivyo basi utajiri wa kutumia ufisadi kwa
kujitajilisha haukubariki hata kidogo, na machozi ya watanzania yatawafuata
mpaka huko kaburini, Japo serikali inayoongozwa na Rais John Pombe magufuri
haitasubiri mpaka ufe, bali tutawatumbua wakiwa hai.”
Lakini pia ameshauri NBAA kuwafuta na kuwafukuza
wale wote wanaojiusisha na tabia ya kifisadi na kutafuta utajili kwa haraka
maana wanachafua kada na taaluma ya
uhasibu.
Post a Comment