Meneja wa kanda (Tanzania) Marry Nkonya akiwakaribisha
wahudhuliaji wa warsha katika hotel Coral Beach jijini Dar Es Salaam.
|
Afisa mipango wa Going for Gold Jenni Sawyer kutoka SIMAVI akielezea nafasi ya shirika
hilo linavyofanya kazi hasa katika nyanja ya kuwawezesha wanawake walio katika
maeneo ya machimbo.
|
Wahudhuliaji wa warsha kutoka mashirika mbalimbali yakiwemo
ya serikali na taasisi binafsi wakisikiliza na kufuatilia.
|
Katibu mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia,
Wazee na Watoto Sehaba Nkinga akisoma risala na kufungua warsha inayoangazia
kumuwezesha mwanamke kumiliki eneo la machimbo.
|
HABARI KWA UNDANI:
Warsha inayoangazia uchumi wa
mwanamke kupitia nyanja ya uchimbaji wa madini nchini, iliyopewa jina kama Going for Gold inamulika katika kumfanya mwanamke kukwea kutoka kutegemea na
kuweza kujitegemea katika tasnia ya uchimbaji wa madini nchini zaidi aweze kuwa
na nafasi kiuchumi.
Katika washa hiyo iliyohuzuliwa na
wawakilishi wa mashirika ya kijamii kama Umati, Salama Heritage, MEM, TAWLA na
mengineyo, pia unaangazia na kulenga katika mpango utakaokuwa na tija huku ikifahamika
wachimbaji wadogo wana nafasi katika kukuza uchumi wa nchi na ushiriki ikiwemo
wanawake waliopo katika nyanja hiyo.
Kwa niaba ya waziri wa Afya, katibu
mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto Sehaba Nkinga
akifungua warsha hiyo jijini Dar Es Salaam anasema; “Mpango
huu umekuwa ukifanyika mkoani Geita ukiwa na kuhakikisha wanawake wanashiriki
kikamilifu katika kazi ya uchimbaji madini, wapo wanawake wanaojihusisha katika
uchimbaji lakini mpango huu unalenga kuwasaidia kinamama waongezeke katika
uchimbaji wadogo wa madini japo wengi wanajihusisha wanakihusisha kwenye
mapishi na uuzaji wa mboga mbaoga.”
Post a Comment