0

Na Bumija Mvungi -ARUSHA.
Mratibu wa Programu za Misitu, Mazingira, Maliasili Duniani wa shirika la World Wildlife Fund [WWF] kwa upande wa Tanzania Isaac Malugu amesema wakati wa mafunzo ya kwanza katika nchi zlizoshiriki zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na Zanzibar.

Utoaji wa mafunzo hayo umelenga kuwajengea uwezo na namna yakutambua mazao ya misitu ambayo ni Mbao, Vinyago na Nguzo za aina mbali mbali kuwa kila zao linatozwa ushuru tofauti na zao lingine pamoja na kutoza mazao katika mipaka ya nchi hizo na kutambua kila zao la misitu linatozwa Ushuru  kiasi gani.

Kwa upande wa Changamoto zinazowakabili amesema Tanzania imekuwa ikipoteza Dolla za Marekani 10 millioni kwa mmoja na  nchi jirani nazo zimekuwa zinapoteza mapato kama hayo na ndio maana wameona umuhimu kushirikisha nchi hizo, kukutana na kijadiri. Aidha baada ya mafunzo hayo wameazimia kufanya tathimini ya mazao ya misitu mara kwa mara kwa kila nchi husika.

Post a Comment

 
Top