Rais John Magufuri. |
Kukosekana kwa maeneo
rasmi ya kufanya biashara ndogo ndogo tayari kumezusha migongano ya mara kwa
mara na kusababisha uvunjifu wa Amani katika maeneo mbali mbali nchini.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali ya kuondoa wafanyabiashara ndogo ndogo
katika maeneo yanayodaiwa hayaruhusiwi hususan kwenye miji mikubwa kama Mwanza,
Shinyanga, Arusha na Dar es salaam na kuzusha vilio na simanzi baada ya mamlaka
husika kwenye miji hiyo kuwaondoa kwa nguvu na kusababisha hasara ya mali zao.
Wafanyabiashra ndogondogo wakiwa eneo la Ilala Dar. |
Kufuatia maagizo hayo ya Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Rais,
tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, George Simbachawene amewataka
wakuu wa mikoa, wilaya na mamlaka ya serikali za mitaa kuwatafutia wamachinga
maeneo rafiki ya kufanyia baishara badala ya kuwabughudhi kwa kuwaondoa katika
maeneo yao wanayofanyia biashara na kuwaingizia kipato.
Rais
Magufuli alisema “Sipendi
Wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara lakini hakuna sheria katika
nchi hii inayosema mtu mwenye biashara ndogondogo au Mmachinga hatakiwi kukaa
katikati ya mji, tukianza kwenda na utaratibu wa namna hiyo maana yake tunaanza
kutengeneza madaraja ya Watanzania, kwamba kuna Watanzania fulani wa daraja fulani
wanapaswa kukaa katikati ya mji na Watanzania wa daraja fulani hawatakiwi kukaa
katikati ya mji, huo sio mwelekeo wetu na wala Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi ambayo mimi na wewe (Makamu wa Rais) tulipita kuinadi, haisemi
tutengeneze madaraja ya watu wanaostahili kukaa mjini na wengine hawastahili
kukaa mjini, sasa nimeona hili nilizungumze na nataka kulirudia kwa mara ya
mwisho.”
Hata hivyo Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana
kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sharia.
Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo
hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye
hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.
Post a Comment