Rais mteule wa Marekani Dornald Trump. |
Baadhi ya viongozi wa mataifa mengine duniani wakipokea kwa mikono miwili
usafiri wa angani kwa matumizi yao wakiwa watawala, rais mteule wa Marekani
Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force
One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.
Serikali ya
Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing kuundiwa ndege mbili au zaidi zitakazotumika kuwabeba
marais, ndege hizo zinatarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.
Aina ya ndege za Boeing ambazo Trump anaeleza kuzikataa. |
Wiki sita kabla
ya kuingia madarakani, aliandika kwenye Twitter: "Boeing
wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku
zijazo, lakini gharama yake ni kubwa sana, zaidi ya USD 4 billioni. Futa oda
hiyo!"
Hisa za kampuni
hiyo ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trump
kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye alasiri, Trump hatarajiwi kutumia
ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili mwaka 2020.
Kwa
sasa anatumia ndege yake binafsi, lakini atakapokuwa rais atahitajika kutumia
ndege za Air Force One, ambazo ni moja ya mipango ya serikali ya Marekani kwa
viongozi wake wakuu wan chi kutumia ndege hizo sababu zimeimarishwa kwenye mifumo
ya usalama, ulinzi na mawasiliano.
Post a Comment