0


Kilimo kimekuwa ni moja ya nguzo kwa nchi zote duniani ikizingatiwa kuwa mfumo wa maisha kwa njia moja tu kwa binadamu anaishi kutegemea mlo unaotokana na Chakula, hivyo basi Kilimo ni sehemu muhimu katika maisha ya Binadamu duniani.

______________________________________
Mwandaaji wa chapa Mkulima Market Vicensia Shule akiongea na TODAYS NEWS wakati wa kutambulisha Mkulima Market.



Kutoka kushoto ni mratibu msaidizi, uhamasishaji, vikundi na wajasiriamali Steven Peter Mfuta katikati Vicensia Shule Mwandaa Soko la wazi, Mkulima Market na mwisho kulia ni Mratibu msaidizi mawasiliano ya Umma Vicent Mirumbe.

HABARI KWA UNDANI:
Kwa mara ya kwanza hapa nchini chapa ya MKULIMA MARKET inatambulishwa huku ikitarajiwa kuleta mapinduzi katika shughuli za masoko hapa nchini, lengo kuu la Mkulima Market inaangazia kuwaunganisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa muda wa siku tatu katika soko la wazi ambalo litafanya wafanyakazi ambao ni sehemu kubwa ya wadau wa bidhaa za kilimo waweze kushiriki kikamilifu.

Uwepo wa soko la wazi ambalo linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar Es Salaam Dec. 23-24.2016 kutawafanya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kupata muda wa kutosha kuona bidhaa mbalimbali kutoka kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wawindaji pia wakifanya manunuzi ya moja kwa moja.

Mwandaaji wa chapa Mkulima Market Vicensia Shule anasema “pamoja na kuwepo kwa soko la wazi kutakuwepo na elimu mbalimbali zitakazotolewa kuhusu ubora wa bidhaa, ufungashaji, ujasiliamali pamoja na mambo mengine, lakini pia kutakuwa na burudani, michezo ya watoto huku tukitoa fulsa kwa watoa huduma mbalimbali kama chakula wakikaribishwa.”

Aidha amegusia gharama za ushiriki ikiwa ni kwa siku moja; Banda dogo 50,000 kubwa shs 100,000 na kwa siku zote tatu Banda dogo shs 125,000 kubwa shs 250,000 pia nafasi kwa washiriki kuchangia banda kutokana na uchache wa bidhaa imetolewa na waandaaji.

Post a Comment

 
Top