0
Rais John Pombe Magufuri.
Watanzania wameendelea kusherehekea kukumbuka siku ya uhuru ambayo Tanzania bara wakati huo ikijulikana kama Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961ambapo kwa mwaka uliopita haikuweza kufanyika kutokana na sababu ambazo leo zimewekwa wazi na Rais Magufuri.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuri ameelezea sababu za sherehe hizo kutofanyika mwaka jana ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kuingia madarakani, ikiwa ni kutokuwepo kwa bajeti ya kutosha kuweza kumudu sherehe zilizopita na badala yake fedha zilizokuwa zimetengwa kufanya sherehe hizo zilielekezwa kupanua barabara ya bagamoyo kuanzia eneo la morocco mpaka makutano ya barabara ya sam nujoma  na bagamoyo (mwenge).

Wakati maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika katika jiji maharufu la kibiashara Dar Es Salaa na kwenye uwanja uliozoeleka wa Uhuru hii ndiyo itakuwa mara ya mwisho kwa maadhimisho haya kusherehekewa jijini Dar Es Salaam na uwanjani hapo, hii ni kutokana na kauli ya Rais Magufuri kuwa maadhimisho yajayo yanatarajiwa kufanyika makao makuu ya nchi mjini Dodoma.


Wakati akitaja majina ya viongozi watangulizi wake waliowahi kushika nafasi ya urais alimtaja Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi ambaye kutokana umri na kiasi kikubwa cha mvi alinazo alimfanisha na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania ndg Edward Lowassa ambaye ana mvi kichwa kizima hivyo basi mzee Mwinyi anaweza kuja kuwa Lowassa wa pili kutokana na mvi alizonazo.
Hali hiyo iliibua kicheko kwa mzee mwinyi pamoja na watanzania waliohudhulia sherehe hizo na wengine kuonyesha furaha.

Hata hivyo Rais Magufuri ameelezea mabadiriko makubwa yaliyopo sasa ambayo ni tofauti na mwaka 1961, kwa sasa nchi imepiga hatua kimaendeleo kupitia sekta mbalimbali wakati hivi sasa serikali inawezeka katika ujenzi mkubwa wa reli ya kisasa (Standard Gauge)ambayo itaanza kujengwa kwa urefu wa 200km ikiunganisha baadhi ya nchi ukanda wa Afrika Mashariki, ununuzi wa ndege 6 ambazo zitaweza kusaidia kukuza biashara ya utalii nchini na tayari tatu zimeanza kutoa huduma.

Upande wa Elimu serikali yake imetenga kiasi kikubwa na bajeti ambapo amesema kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi pamoja na wale wa sekondari, vile vile kwa upande wa Afya napo serikali imetenga fedha za kutosha, kutokana na makusanyo ambayo serikali yake imeongeza kutoka shs 850bilioni mpaka kufikia shs 1,2 Trilioni.

Hata hivyo Rais Magufuri ametoa onyo kwa baadhi ya watendaji mafisadi na wala rushwa kuwa serikali pamoja na balaza la mawaziri aliowateua hawatamvumilia kiongozi yeyote atakayekwenda kinyume na matarajio na wataendelea kuwatumbua hadharani na amelishukuru Bunge kupitisha sheria ya kuwashitaki katika mahakama maalum wale wote watakaohusika.

Pamoja na hayo amegusia wafanyakazi hewa wapatao 19,000, familia hewa zipatazo 55,000 ambazo TASAF imekuwa ikiwalipa, wanafunzi hewa wapatao 65,000 wote hawa wamekuwa wakirudisha nyuma hatua ambazo serikali imekuwa ikipiga katika kuboresha maisha ya Watanzania.

“serikali yangu kupitia mawaziri mpaka makatibu kata imepanga kuondoa uonevu hasa unaofanywa kwa wananchi wanyonge” alisema Rais Magufuri.

Amewataka watanzania kudumisha Amani ya nchi, ushirikiano ikiwa hakutakuwa na amani basi hakutakuwa na maendeleo hivyo inatakiwa kilinda maana ndiyo nguzo hata hivyo hakuacha nyuma kuwataka watanzania kuulinda Muungano wan chi mbili kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

“watanzania tufanye kazi kama msemo wa hapa kazi tu, nawaomba tufanya kazi mimi pamoja na waziri mkuu na balaza la mawaziri tutafanya kazi kwa watanzania wote pasipo kubagua chama” Alimaliza kusema Rais Magufuri.

Post a Comment

 
Top