Huduma ya Afya inasemwa kuwa ni moja
ya sehemu ambayo mtoa huduma hapaswi kuweka faida au maslahi mbele, eneo hili
linatajwa kuwa ni sehemu ambayo utu unapaswa kutangulia kabla ya vitu vingine.
Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta alivunja ukimya wake mnamo Jumatano katika mgogoro huo na kuwataka madaktari kurudi kazini kuyapa nafasi mazungumzo baina ya chama cha madaktari na serikali.
Madaktari, wauguzi, famasia, madaktari wa meno na wataalamu wengine wa afya ambao idadi yao inafika 5000 wamesitisha huduma za afya na kuathiri vituo vya utoaji huduma za afya zaidi ya 2700 nchini Kenya ambapo wagonjwa wamelazimika kwenda kutafuta huduma hiyo kupitia hospitali za binafsi.
Inaripotiwa kati ya watu 14 mpaka 20 wamepoteza maisha kutokana na mgomo wa madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Kenya mgomo ambao unaingia siku ya nne tangu uanze.
Akizungumza katika uzinduzi wa chuo
cha Madaktari mjini Makindu, mashariki ya Kenya, Rais Kenyatta alisema: “ni lazima tuwe
na huruma na maisha ya wananchi wenzetu, ni kwa nini tumekubali zaidi ya watu
14, au karibia 20 kupoteza maisha, kwa wafanyakazi wa umma, hasa madaktari na
wauguzi waliogoma hakuna kiongozi wa serikali aliyekataa kuzungumza nao. Nyote
mmeshuhudia katika masiku machache yaliyopita, tumekuwa tukifanya kila tunaloweza
kumaliza mgogoro huu,”
Dr. Ouma Olunga ambaye ni
mmoja wa madaktari aliyejiunga kwenye mgomo alisema: “sisi kama madaktari, tunataka haya
makubaliano yatimizwe na madaktari walipwe malimbikizo yao ya miaka mitatu iliyopita.”
Waandishi wa Sauti
ya Amerika walioko Kenya wameripoti kuhusu
wagonjwa kukosa matibabu katika hospitali za Mombasa, Kisumu na Nairobi pamoja
na huduma za matibabu kusitishwa katika hospitali za umma kote nchini kufuatia
mgomo huo.
Post a Comment