![]() |
Mchungaji Kombo akimbatiza mtoto Comfort Innocent
Moshi wakati wa ibada ya krismasi katika kanisa la Kiinjili la kilutheli usharika wa Boko jijini Dar eS Salaam. |
Tukio la kuzaliwa Yesu Kristo miaka
zaidi ya 2000 iliyopita, limekuwa likisherehekewa na kuadhimishwa na baadhi ya
wakristo duniani kote (tunasema baadhi ya wakristo ikiwa na maana kuna baadhi
wasioamini kuzaliwa kwa kristo disemba 25.12.) Na sehemu ya wakristo wasiomani tarehe hizo ni waadventisra wasabato.
Hivyo
basi nchini Tanzania tukiwa ni sehemu ya dunia watanzania wamesherehekea
siku hiyo pamoja na kuwepo changamoto mbalimbali baadhi wakidai zinatokana na ukata wa fedha
ikiwa ni tofauti na miaka iliyopita, hali hii inasemwa inatokana na mazingira
yanayochagizwa na hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kipindi hiki.
TODAYS
NEWS ilipata nafasi ya kuhudhulia moja ya ibada katika kanisa la kiinjili la kilutheli
ushirika wa Boko jijini Dar Es Salaam ambapo katika misa ya krismasi iliyoendeshwa
na mchungaji Boniface kombo ambaye ni naibu katibu mkuu wa dayosisi ya mashariki na pwani ametoa wito wa kuwa na Amani kutokana
na Yesu alipozaliwa alikuja kuunganisha na si kubomoa, hivyo basi kila mtu ana
wajibu wa kutambua ikiwemo kusherekea huku akiwa na wajibu wa kutunza amani.
Katika
kuonyesha umuhimu wa Amani nchini, afrika na duniani, sauti ilisikika ndani ya
kanisa hilo la KKKT DMP –Boko kutoka kwa kwaya kuu ya kanisa hilo ilipokuwa
ikiimba wimbo unaoitwa ‘MAANA KWA AJILI YETU’ ambao moja ya beti zake zilisikika zikisema; **Tanzania
yahitaji sana mtawala wa Amani na magombano yasiwepo, katika nchi yetu tumwombe
sana Mungu ufalme wake ushuke (ili tuishi kwa Amani siku zote) maishani mwetu’
aliyezaliwa mfalme wa Amani, Amani twahitaji, Tanzania Afrika na dunia nzima
iokolewe.


Post a Comment