Profile photo: Ben Saanane. |
Sakata
la kutoweka kwa, Ben Saanane limechukua sura mpya baada ya chama cha demokrasia
na maendeleo nchini kutoa tamko kwamba hawajui alipo msaidizi huyo wa
mwenyekiti wa taifa wa chama hicho upande wa siasa na jamii.
Kupitia mwanasheria mkuu wake
Tundu Lissu, chama hicho kimeitaka serikali kupitia jeshi la polisi kufanya
uchunguzi wa kina juu ya mahali alipo Ben Saanane, anayedaiwa kutoweka tangu mwezi
uliopita wa novemba 14.2016, mara ya mwisho kupata taarifa zake inadaiwa
aliwasiliana na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Mwanasheria
wa chama hicho Tundu Lissu amesema serikali ndio yenye ulinzi na udhibiti
mkubwa wa mipaka ya nchi ambapo inao uwezo wa kufahamu kama mtu ametoka nje ya
nchi au yupo ndani ya nchi hivyo wanawajibu wa kufanya kila njia ya kumpata Ben
ambaye taarifa za kutoweka kwake kwa mara ya kwanza zilitolewa na ndugu zake wa
karibu.
Tundu Lissu alisema “Wakisema
wamemkamata tutawauliza kwa nini wamemkamata na kumshikilia muda wote.
Hatumtuhumu mtu yoyote tutauliza masuala ambayo yanahitaji kuulizwa”.
Post a Comment