Mnyama aina ya Faru. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atoa siku kadhaa kupewa taarifa.
Tanzania imebahatika kuwa moja kati ya nchi zenye
maliasili nyingi na vivutio vya kila aina huku wakiwepo wanyama wa aina
mbalimbali wanaopatikana hapa na kutokuwepo mahali pengine duniani.
Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo ambalo linavutia
kutalii na dilo eneo pekee nchini ambapo mnyama aina ya faru wanapatikana kwa
wingi porini, ngorongoro ipo ndani ya kreta, inakadiriwa idadi ya faru waliopo katika
hifadhi hiyo ni takriban 35.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
|
Katika ziara yake hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka maafisa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
HABARI KWA UNDANI:
Bw Majaliwa amewataka
viongozi wa Ngorongoro kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika kumuhamisha
faru huyo kufikia alhamisi ambapo alisema ana taarifa kuwa faru huyo
alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti kwenye eneo la Serengeti mnamo
17.12.2015.
Waziri mkuu alisema "… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200
ambapo mkapewa shilingimilioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100
nyingine baadaye,"
Kwa mujibu wa gazeti la
Daily News Waziri mkuu Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa
zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa ila alisisitiza kwa kusema; "Naomba niletewe nyaraka zote
zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili
suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo
itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa
hatua kali za kisheria,".
Katika hatua nyingine Mh.
Majaliwa pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa hifadhi ya Ngorongoro Sezzary
Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili. Sezzary kwa
sasa, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani
mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga
uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na
aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini," Mh. Majaliwa alisema.
Post a Comment