HABARI KWA UNDANI:
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Bodi ya wadhamini, menejimenti na wafanyakazi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kunga mkono jitihada na kumpa moyo,
kumpongeza Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri
katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala toka kuapishwa kwake taifa.
Wakati akifanya ziara mnamo mwezi November 9.2015
siku nne baada ya kuapishwa mh. Rais alifanya ziara hospitali ya Taifa ya
muhimbili na kukutana na changamoto kadhaa ambapo alitoa maagizo kwa uongozi wa
hospitali kukarabati mashine ya magnetic Resonance Imaging (MRI) na
Computerized Tomography Scan (CT Scan) ziwe zinafanya kazi katika kipindi cha
siku 14 pamoja na wagonjwa waliokuwa wanalala chini wawe wamepatiwa vitanda na
wagonjwa kuhakikishiwa kupata dawa hospitalini hapo.
Ili kuonyesha mafanikio ndani ya kipindi hicho
mashine, vitanda na upatikanaji wa dawa ulifanikiwa, huku ikiendelea kuboresha
huduma mbalimbali hospitalini hapo ambapo kwa upande wa wagonjwa wanaofika
kutibiwa na kuondoka (OPD) jitihada zimefanyika na kuweka mkakati wa kuanza
kliniki saa 03:00 asubuhi, huku kukiwa na kliniki kwa siku za jumamosi na siku
za sikukuu.
Pamoja na hayo upasuaji umekuwa ni wa kasi ambapo kila
siku jumatatu mpaka ijumaa wagonjwa 40-50 wamekuwa wakipatiwa huduma hiyo,
wakati kabla ya hapo ilikuwa unafanyika chini ya wagonjwa 10. Wakati huohuo
maabara imeongeza vifaa vya kisasa katika kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa
ubora wa juu.
“Wakati huduma zikiwa zinaonyesha
ufanisi, mapato pia yameongezeka kwa asilimia 100, takwimu zikionyesha wastani
wa shs bilioni 4.6 kwa mwezi kutoka wastani wa shs bilioni 2.3 ilizokuwa
ikizalisha hao awali, haya ni mafanikio makubwa sana kwa upande wa mapato kuwahi
kupatikana katika kipindi kifupi cha miezi miwili tu”, anasema
Aminiel Aligaesha, mkuu wa mawasiliano ya umma
MNH.
Hata hivyo mafaniko hayo, kero za wafanyakazi na
morali ya kufanya kazi, rufaaa za wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu,
usimamizi wa utendaji kazini, ikiwa ni pamoja ulipaji wa madeni ya wafanyakazi
umeonekana kwa kipindi hicho huku matumizi yakishuka kutokana na kuagiza madawa
moja kwa moja kiwandani, miundombinu, yote hayo yanaonekana kupata ufumbuzi
katika kuhakikisha mafanikio.
Pamoja na hayo, mipango ya muda mrefu na muda mfupi
ipo mbioni ili kuhakikisha mafanikio zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia mfumo wa kuona
wagonjwa katika OPD zote, kununua vifaa
vya upasuaji kwa ajili ya vyumba vya upasuaji, kulipwa kwa madeni, kupunguza
idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje, kusomesha wataalam zaidi,
kutembelea hospitali kadhaa nchini ili kutoa mafunzo, kuongeza mapato mpaka
kufikia shs bilioni 5 kwa mwezi ifikapo Julai 2017.
Post a Comment