0
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) Martin Munisi  wa wilaya ya Arusha mjini ameliomba jeshi la polisi kumkamata mara moja mbunge wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha Chadema Godbless Lema kwa kitendo chake cha kumkashifu na kumtamkia Rais Magufuli kuwa atapoteza uhai kabla ya 2020!.



Mwenyekiti huyo Martin Munisi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio kilichopo jijini humo, huku mbunge huyo akisisitiza kama hatawasikiliza chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)


Mwenyekiti wa UVCC Arusha Martin Munisi
Katika hatua nyingine Munisi amelitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi wa mikutano iliyokatazwa na inayotakiwa mbunge huyo anafanya mikutano ya chama chake na siyo mikutano ya mbunge kama inavyofahamika na ambayo inatofautiana na ahadi za mbunge kwa wananchi kupitia chama chake.

Mikutano ya mbunge hulenga kuzungumzia ahadi za mbunge alizotekeleza, atakazotekeleza na kuhamasisha maendeleo ila kinyume chake Lema yeye anasema wananchi wataingia barabarani maana hali ni mbaya mara raisi takufa kabla ya 2020

“haya ni maneno yasiyovumilika hata kidogo kwenye jamii iliyostaharabika ni vizuri jeshi letu likamhoji mbunge lema kuhusu kumzushia au kutabiri kifo kwa mwenyekiti wetu wa chama, taifa na Rais wetu, kwa vile Lema hana agenda na nalitaka jeshi la polisi kuzuia mikutano yake kama wasipozuia sidhani kama vijana wa ccm na wananchi wapenda nchi yao watakuwa tayari kuvumilia matusi ya lema kwa mh Rais, wetu mpendwa” alisema Martin Munisi.

Post a Comment

 
Top