0

Baadhi ya matukio katika picha zikionyesha viongozi hao wa zamani wa chama cha mapinduzi katika matukio tofauti mjini Dodoma mapema leo.


Aliyekuwa  mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa na Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye leo asubuhi wamehudhuria Bungeni ikiwa ni siku ya kwanza tu ambapo kikao cha kwanza cha mkutano wa tano wa Bunge la 11, mjini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa Chadema wakiongozwa na Aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowasa aliyekunja mikono kidevuni na Fedrick Sumaye aliyekaa kulia juu, wakiwa bungeni dodoma.

Mawaziri hao wastaafu waliokihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA inasemekana walikwenda mjini Dodoma kutoa somo kwa wabunge wa UKAWA jinsi ya kukabiliana na wabunge wa CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.

Post a Comment

 
Top