HABARI KWA UFUPI.
Leo Rais Magufuli amekuwa
na mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari nchini na kuuelezea mwaka mmoja wa
kuwepo kwake madarakani ambapo alitoa muda kuulizwa maswali ambayo aliyajibu
moja kwa moja.
Katika mkutano huo na amesema mpaka sasa anendelea kutimiza malengo huku makusanyo yakiongezeka kutoka bilioni 800 kufikia trillioni 1.2, pia amegusia ununuzi wa ndege katika hilo amesema ni vigumu kujenga utalii pasipo kuwa na ndege zenye safari za uhakika nchini, na kuongeza kuwa mpaka sasa zipo tatu na nyingine inatarajiwa kuja mwezi wa sita ili kufikia saba.
Rais alipata nafasi ya kuongelea suala la kilimo ambapo katika nyanja hiyo anasema wawekezaji kadhaa wameanza kuja huku wakulima wakianza kuona matunda ya uwekezaji katika nyanja hiyoambao ni muelekeo mzuri katika uti wa mgongo wa taifa. Hakusita kutolea mfano kilimo cha korosho zinazolimwa kwa wingi mikoa ya kusini kuwa kwa sasa bei ya korosho imepanda kutoka shilingi 1000 na kufikia shs 4000 kwa kilo.

Kwa upande wa nishati anasema serikali imetenga bajeti kiasi cha trilioni 1.3 kwa
mwaka huu na kwenye elimu bajeti yake kwa mwaka huu ikiwa ni 4.47 wakati
anaingia hakukuwa na bajeti ya mfumo wa elimu kutolewa bure lakini walitoa makusanyo
ya ziada kugharamia elimu hiyo japo kuna changamoto kadhaa.
akizungumzia mfumuko wa bei ambao amesema umeshuka kutokea asilimia 7 hadi 4.5, japo watu watauliza mbona pesa hakuna na lakini zitaendelea kutokuwepo kwa watu ambao ni wapiga dili, maana kuna watu walikula sana miaka ilioyopita na kujisahau, zile pesa za chai na malupulupu kwa sasa hazipo na ndiyo hizo zilizokuwa zinawapa watu kiburi.
Aliendelea kusema “kulikuwa na safari za hovyo hovyo za watu kupishana angani na nimeanza mimi, nilialikwa mikutano 47 ila nimeenda 3. Pamoja na kufanya hivyo bado marafiki zetu wametuheshimu na kuja kututembelea, hata hizo safari za nje nimekuwa nikiwakilishwa vyema na makamu wa Rais au mabalozi wetu kule walipo.
Akijibu swali kuhusu upatikanaji wa dawa ikiwa watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, Rais mMagufuri anasema “Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na tumeongeza bajeti ya kununulia madawa mara kumi zaidi lakini pia tumebadilisha utaratibu badala ya kununua kutoka kwa msambazaji, kwa sasa tunanunua moja kwa moja kutoka kiwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda vya kutengeneza madawa hapahapa”.
Pia amezungumzia tatizo kubwa la ujangili ambalo amesema kiukweli ni changamoto ila pia ina historia yake, katika sheria ya mifugo ya mwaka 59 ila tumejipanga kuhakikisha haya masuala yasije yakawa ya kudumu na ndiyo maana tumeibadilisha wizara ya maliasili na nimeteua majenerali kuongoza wizara hiyo hivyo tunataka kufanya kitu tofauti.
Kuhusu madini, anasema ni kweli nchi hii ina madini mengi sana, madini yanatakiwa kunufaisha nchi hii, siku moja yatakwisha, nina uhakika sasa mambo yataanza kwenda vizuri baada ya kusaini kanuni. Nchi yetu iuna mafuta lakini pia tutaunganisha bomba la mafuta la hoima kutokea Tanga, madini ya Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini nchi iliyoongoza kuuza ni India ikifuatiwa na Kenya. Sasa hivi umeanzishwa mnada hapa.
Watu wanasafirisha makontena kwenda nje kusafishwa na sisi wenyewe tunayasindikiza.
Kwa nini tusitengeneze hapa, haya ndio ndio najaribu kuyazungumza ili nchi yetu isiendelee kuibiwa, kwa nini kila sehemu kwenye madini kuna kiwanja cha ndege, hili sio suala la Rais pekee kwani pesa zinazopatikana zinawanufaisha watanzania wote. Unachosema ni sawa na kinachotakiwa sasa ni kusonga mbele.
Katika hatua nyingine Rais Magufuri ameelezea nia yake ya kuleta maendeleo kwa watanzania wote pasipo kujali dini, kabila au hata chama cha siasa akitanabaisha huu ni muda wa kufanya kazi na kuwaletea watanzania maendeleo na hakasisitiza kuwa "sikuja kufukua makaburi, maana mengine naweza kushindwa kuyafukia" hivyo yapaswa kusaidiana katika kila hatua ya maendeleo inayotakiwa kwa watanzania.
Post a Comment