Mkurugenzi mkuu wa JAVIS Haron Elius Marwa. |
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Ni miongo kadhaa
kumekuwepo na vijana wengi wanaomaliza masomo na kukaa kudai kutopa kazi hama
biashara ya kufanya, hali hii inatokana na mara kadhaa wasomi wengi wanaomaliza
masomo wana mawazo ya kumaliza elimu ya juu au ya kati wakitambua kuna ajira pindi
wawapo nje ya masomo.
Mnano mwaka 2014 mmoja
kati ya watanzania wengi waliopo nchini na nje ya nchi Haroun Elias Marwa alisajili
kampuni inayowaunganisha wafanyabiashara wa nchini Tanzania na wale wa nchini
China ijulikanayo kwa jina la JAVIS INTERNATIONAL TRADE COMPANY
LIMITED kwa lengo la
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora na ikiwa na nia ya kutenheneza jamii ya
kisasa katika mfumo wa biashara.
Kampuni hii ina makao
makuu yake katika mji wa Yiwu na ofisi katika mji wa Guangzhou ambapo
inawaunganisha wafabiashara watanzania wenye mtaji mkubwa na mdogo ambao
wameanza kuwatambua kutokana na utendaji wao.
Kwa maneno ya Leon John
Mwangakala JAVIS inajipanga kutoa huduma yenye kulenga kuleta mabadiriko katika
tasnia ya biashara nchini, huku ikiongozwa na vijana wenye nia na kutafuta njia
mbalimbali zenye kuleta tija, mfano huko ulaya vijana ndio wanaoleta mapinduzi
katika mfumo mzima wa maisha, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tuna uhakika wa
kufika pale kwenye kilele cha mafanikio.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Javis International Harun Elius Marwa |
“Tunatoa cheti kwa
bidhaaa unazonunua pia tukitoa bima kwa mzigo ulionunua huku asilimia kadhaa ya
pesa ikirudishwa kutokana na kupotea kwa mzigo wako kabla haujakufikia na hii inafanyika
pale tu kunapokuwa na itilafu yoyote ya uharibifu” anasema Meneja masoko
wa Javis Steven Gerald.
Anaendelea kusema “kampuni hii inatoa huduma mbalimbali za kifedha huku
ikiwa na ushirikiano na mabenki ya kifedha nchini china, njia mbalimbali za
malipo ya kifedha zikitumiaka, faida inayopatikana kwa kutumia huduma za
kifedha kupitia kampuni au mabenki haya ni pamoja kulipa nusu ya fedha na unapopokea
mzigo unamalizia kulipa”
Post a Comment