Kushoto ni tikitimaji la asili na kulia ni tikiti maji lililoboreshwa. |
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Pamoja na kuwepo kwa utafiti kila uchao,
ikiwepo uzalishaji wa vyakula vitokanavyo na mimea kama mahindi, ngano, miti ya miembe
inayozaa kwa muda mfupi nk, ni muda sasa kumezuka aina ya tafiti zinazoelezea
ubaya wa kila kitu hususani aina fulani ya vyakula (kwa wakati huu) huku
ukisisitiza kuwa kila unapoendelea kula aina hiyo ya basi tegemea kupata
madhara ya aina fulani.
Bahati
mbaya watafiti wa hizo tafiti asilimia kubwa ni wakoloni/wazungu na mimi
niliyetawaliwa naendelea kutawaliwa kifikra kwa kubeba tafiti hiyo kwa
uhaminifu kwamba ipo sahihi pasipo kujua njia gani imetumika kupata uhakika wa
tafiti hiyo au nani anahusika kuruhusu upandikizaji hofu kwa jamii.
Kwa
muda sasa mazao ya asili yanatoweka, jambo la kushangaza hata kwenye miji
mikubwa kama Dar Es Salaam tena katikati ya jiji, utashangaa kukuta mmea
unaliwa na wadudu jamii ya panzi ambao ukijiuliza wametoka wapi mpaka kufika
eneo hilo tena kufuata mmea mmoja tu unaweza kushangaa wakati ukiendelea ukijiuliza!.
Inasemekana
matunda jamii ya tikitimaji la awali/asili ndiyo limeanza safari ya kutoweka
huku likipigiwa upatu wa kutofanya vizuri sokoni (kukosa soko) na kuwa na garama
kubwa kulihudumia tofauti na tikitimaji la kisasa ambalo linapewa nafasi ya
kufanya vizuri sokoni na kukubalika nchini na kimataifa, lakini bado watafiti
(watawaliwa) hawajatoa faida na hasara kwa tunda hilo!.
Kushoto ni Ndoa ya watu wa jinsia mbili tofauti inayohakisi ukweli na kulia ni muungano usio sahihi wa jinsia moja. |
Lakini
kuna suala ambalo limeshika kasi kutokea huko ughaibuni mfano kwa askari ambaye
ni shoga anapewa nafasi kutoka kwenye gwaride kwenda kuweka nadhiri ya uchumba
kwa kijana shoga, hapa lazima ukiwa binadamu wa kawaida mwenye kuhisi njaa na
ukahitaji chakula ili ule lazima ushituke katika hili, kwa nini hii?
Kuna jambo
nyuma ya pazia ambalo hujui hila ya tukio hilo na umeletewa mbele ya pazia kama
ndiyo uhalisia na hali halisi, hivyo linapokufikia popote ulipo na kukupa
uhalali wa wewe kutofanya tafiti na hata kutumia akili yako kwa nafasi ndogo,
ila linakupeleka kuona huo ndiyo ukweli kwa maisha haya.
Bado
tuna nafasi ya kutafakali na kuchuja kila utafiti unaoletwa mbele yako ili
kukuepusha kuwa mmoja wa wanaoeneza propaganda hasi za kutisha na kuiweka jamii
njia panda katika matumizi ya vyakula ikionyesha hatari, huku kila aina ya
vyakula vya asili vikiendelea kubadilishwa kuonekana havina uwezo tena wa
kuimiri hali ya mabadiriko ya kimazingira katika tabia nchi.
Post a Comment