File: Wahamiaji ambao wamekuwa wakiokolewa kutoka kwenye ngalawa zao mara kadhaaa wamekuwa wakipoteza maisha. |
Katika kuendelea kutafuta maisha nje ya makazi na
maeneo yaliyozoeleka, bado kuna watu zaidi katika nchi za Africa wanokwenda
kutafuta maisha hama makazi nje ya bara hili, inasemekana zaidi ya wahamiaji
239 wanaaminika kufa maji walipokuwa wakisafiri wakitumia ngalawa mbili katika pwani
ya nchi ya Libya.
Hali
inaonyesha mpaka kufikia muda wa saa 1500 alasiri hakuna maiti yoyote
iliyopatikana hata sasa. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa
UNHCR lilipewa taarifa kuhusu tukio hilo na watu wawili walinusulika ambapo
walipelekwa katika kisiwa cha Lampedusa kwa huduma.
File:Moja ya tukio yanayoonyesha wahamiaji walivyojaa kwenye chombo. |
Inasemekana
zaidi ya wahamiaji 4200 wamekufa walipokuwa wanajaribu kufanya safari za kuvuka
bahari ya Mediterranean ambapo ni sehemu ya hatari kwa mwaka huu na kwa mwaka
huu wahamiaji wapatao 330,000 wamevuka bahari ikilinganishwa na zaidi ya
wahamiaji milioni moja mwaka uliopita wa 2015.
Hata huvyo umoja wa mataifa
umetoa onya kuwa, kwa mwka huu unaoenda kuisha 2016 ndiyo utakuwa wenye kuwa na vifo vingi
vilivyotokana na wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari kwa kutumia vyombo vidogo
visivyoweza kukabiliana na hali mbaya hewa.
Post a Comment