0
Wanafunzi wa shule hizo wakiimba nyimbo/ngonjera katika hafla hiyo juu ya elimu bora inayotakiwa kupewa wanafunzi, lengo ni kufikisha ujumbe kwa wazazi na viongozi ili wapewe nafasi zaidi kufikia malengo yao.
Mwenyekiti bodi ya elimu shule za Almuntazir Imtiaz Lalji akiwakilisha hotuba kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa kukabidhi madawati yenye thamani zaidin ya milioni 20 katika moja ya shule hizo Upanga jijini Dar Es Salaam.
Kutoka kulia kwenda kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, Azim Dewji, Sheikh wa mkoa Alhad Musa, Riaz Bhojan wakisiliza baadhi ya mashairi wa wanafunzi.

Baadhi ya wazazi, walimu na wanafunzi waliohudhulia hafla hiyo wakisikiliza kwa makini maneno ya mwenyekiti wa bodi ya elimu wa shule za Almuntazir.





Mwenyekiti wa Khoja shia Ithna Asheri Jamaat Azim Dewji (pichani kulia) akiongea mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo shule hizo zimepitia mpaka kufikia hapo ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam kupewa eneo lenye ukubwa wa nusu eka kwa ajili ya kujenga shule maalum kwa ajili ya watoto wenye usonji.








Baadhi ya madawati ambayo yatakwenda kutumika katika shule za msingi na sekondari nchini hususani kwa mkoa wa Dar Es Salaam ambayo yamekabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaamm mapema leo.
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akikata utepe kuashilia kupokelewa kwa madawati hayo yenye thamani ya shilingi milioni 20, ambayo yatasambazwa kwenye baadhi ya shule zenye upungufu wa madawati jiji Dar.



Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akinyanyua juu mkasi mara baada ya kukata utepe uliokuwa umefunga madawati hayo kisha kuyapoka kwa ajili ya matumizi ya shule za msingi na sekondari nchini kwa mkoa wa Dar Es Salaam kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi ya elimu ya shule za Almuntazir nchini na kulia kwa mkuu wa mkoa ni sheikh wa mkoa wa Dar Es Salaam Alhad Mussa, nyuma anayepiga makofi ni Mbunge Philipo Mulugo ambaye ni Mshauri na mlezi wa shule binafsi nchini (TAMONGSO) wakishuhudia tukio hilo.



Waliokaa katika moja ya madawati kuonyesha uimara kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda, kulia aliyekaa ni Azim Dewji wakionyesha ubora na utayari wa matumizi wa madawati hayo kwa matumizi ya watoto wa shule za mkoa wa Dar Es Salaam.


HABARI KWA UNDANI.

Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Kufuatia agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuri la kuhakikisha halimashauri zote nchini, zinahakikisha shule za msingi na sekondari zinajitosheleza kwa madawati kwa  mwaka huu 2016, wadau mbalimbali wameendelea kumuunga mkono Rais ili kuweza kufikia lengo hilo nchini.

Nchini historia ya shule za awali nchini hutaweza kuacha kuitaja Almuntazir ambazo ni shule kongwe nchini, ambapo shule ya awali ilianza kwa kuwa na shule ya awali/chekechekea kwa zaidi ya miaka arobaini (40) iliyopita, ikianza na wanafunzi wasiozidi 150 mwaka 1975. Ambapo mpaka sasa kukiwa na shule 6 zikiwa na jumla ya wanafunzi zaidi ya 4500 na wafanyakazi zaidi ya 500 wakiwemo walimu.

Katika hafla ya kukabidhi na kutekeleza kwa vitendo juhudi za Rais, mwenyekiti wa bodi ya elimu kwa shule za Almuntazir Imtiaz Laiji amempongeza Rais kwa juhudi zake katika sekta ya eli pamoja na suala la ukosefu wa madawati kwa nchi yenye misitu mikubwa ambayo inaweza kusafirisha magogo nje ya nchi ikiacha watoto wake wakisota kwenye sakafu za vumbi katika mbio za kutafuta elimu.

Wakati wamiliki wa shule hizi ni taasisi ya dini, Imtiaz anasema “udini na ubaguzi haupo shuleni kwetu, kwani wanafunzi wa madhebu tofauti ya dini zote wanaruhusiwa kusoma katika shule zetu, huu ni mfani mzuri wa ushirikiano kwa kuwa wote tumeumbwa na Mungu mmoja, kwa upande wa elimu shule imejpanua na kupigiwa mfano, ikiwa ni shule ya mwanzo isiyokuwa ya serikali ambayo imeanzisha kitengo cha watoto wenye ulemavu wa usonji, ambacho kina wanafunzi zaidi ya 80 ambacho kinasaidiwa na walimu wenye uzoefu mkubwa”

Hata hivyo penye maendeleo hapakosi changamoto, pamoja na kutoza ada ya kawaida mil2.5 shule hizi zinaendelea kutii agizo la wizara ya elimu kuhakikisha ada inakuwa chini ikiwa ni kutoa nafasi ya watanzania/wazazi kupendekeza eneo la kuwapeleka watoto kupata elimu.

Naye sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alisifia shule hizo pamoja na kuonekana kwa changamoto zinazotokana na baadhi ya wazazi, lakini amesema “mti wenye matunda ndiyo upigwa mawe, ukiona mti haupigwi mawe lazima ujiulize, lakini pia baadhi ya waislam wanaojiita wenye Imani kali, wasiopenda umoja na mshikamano baina ya waislam na madhehebu mengine hao siyo waislam sahihi, mimi nina namna yangu ya kushugulika nao nikiwa kama sheikh mkuu, naweza kuwasomea Albadiri ili wapate funzo”

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salamm Paul Makonda ambaye alikabidhiwa madawati hayo amesisitiza utolewaji wa elimu bora huku akiweka mkazo kwa walimu na wanafunzi kwa mkoa Dar Es Salaam watakafanya vizuri kwenye ufaulu wa juu kwa masomo ya sayansi, atawapatia zawadi ya fedha taslim huku wazazi wa mtoto husika wakipata nasafi ya kwenda kutembelea moja ya mbuga wa wanyama nchini wakiwa wamelipiwa kila kitukwa siku mbili.


Vilevile alisonda kidole wazazi wanaopeleka malalamiko yao ngazi za juu huku wakiacha kutumia viongozi walio ngazi za chini kuweza kutatua malalamiko yao, kauli hiyo imekuja baada ya kuonekana baadhi ya wazazi kupeleka lawama shuleni za shule hiyo wizarani hata kabla ya kufikisha kwa afisa elimu wa wilaya ambaye ana mamlaka akiwa kama kiongozi.

Post a Comment

 
Top