Makofi
ya kuonyesha warsha inaanza rasmi, ni wadau, viongozi wa taasisi mbalimbali
wakionekana katika hali hiyo mara baada ya ufunguzi.
|
Picha
ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu za hapo baadaye iliyopigwa muda mfupi baada
ya hotuba ya ufunguzi kabla ya warsha kuendelea, jijini Dar Es Salaam New
Africa Hotel.
|
HABARI KWA UNDANI:
Warsha ya wadau wa
kilimo ulioratibiwa na Mpango wa maendeleo ya kina Afrika –CAADP umewakutanisha
wadau wa pande hizo ikiwemo wizara ya fedha, wizara ya mipango, wafugaji,
taasisi na vyama mbalimbali ukiwa na lengo la kuangazia nyanja mbalimbali
zinazoathiri mafanikio tarajiwa katika ardhi na kuleta hatua nyingine inayoweza
kuleta faida kutokana na aridhi. Hapa kwa mara ya kwanza mwaka 2004 shirika la
chakula duniani (FAO) lilikuja kuipitisha Tanzania katika mfumo huu CAADP.
Warsha hiyo unaoungwa
mkono na mashirika ya kimataifa yanayohusika na kilimo na aridhi kama CARE INTERNATIONAL,
OXFARM pamoja na IFAD, CAADP imekuwa ikiunga na kutoa mfumo wa ukuaji wa
uchumi, usalama wa chakula kwa njia ya mabadiriko ya sekta ya kilimo, bado
kupitia aridhi maendeleo kupitia uchumi mkubwa kwa njia ya kilimo imeonekana ni
ndoto kutokana na mfumo wa mazingira unaotumika kwa kutegemea neema ya Mungu
kwa upande wa mvua haujaleta mabadiriko.
Maria Marialle Mratibu
wa kitaifa wa mradi umiliki aridhi;
anasema “katika kutekeleza tamko la mkutano
mkuu wa viongozi wa umoja wa Africa uliokutana ili kuhainisha changamoto za
ardhi na matatizo mengine yanayohusiana na ardhi, kilimo kimeonekana kushindwa
kutoa jawabu la kile kilichokusudiwa.”
Maeneo mengi katika
nchi za afrika na katika maeneo ya vijijini wananchi wanakijiji wamekuwa hawana
hati ya umiliki wa aridhi wakati mwekezaji anayekuja kijijini anaweza kupewa
hati hiyo ya kumiliki aridhi, hali hii inafanya kudumaza maendeleo na kuwafanya
wananchi walio vijijini kushindwa kuwa na maendeleo makubwa kwa kutumia aridhi
ambayo hawana umiliki nayo.
Magreth Ndaba –Mchumi
na Mratibu wa mashirika ya maendeleo na mashirikiano ya kimaitaifa wizara ya
Kilimo mifugo na Uvuvi, wakati huo huo ni Afisa kiungo wa CAADP nchini anasema
pamoja na mpango anaosimamia kwenda kwa kujongea taratibu, lakini mafanikio ni
mazuri, “katika mfumo wa upatikanji wa aridhi (Land
Access) kwa makundi yote siyo lazima uwe kwenye chama, ila kwa sasa
tunajitahidi vijana waingie kwenye kilimo na tunaangalia upatianaji wa aridhi
kwa ajili ya kinamama na mukundi mbalimbali.”
Pamoja na hilo
inafahamika kuwa aridhi ndiyo mwajili mzuri kuliko mwajili yoyote endapo
itatumika vema ikiwa ni kutumia utaratibu wa njia ya kuipata na kuindeleza,
maana sehemu hii ndiyo yenye kukuhakikishia usalama na kutupatiwa malighafi kwa ajili ya viwanda na
kuendesha sehemu ya ajira kwa vijana wa Tanzania, mifumo na taratibu za kuweza
kuindeleza, kuitunza aridhi lazima iwekwe kwa ajili ya kufikia malengo ya nchi,
malengo yaliyopo na yaliyowekwa na wadau (Afrika) wa kanda na baadaye
kimataifa.
Post a Comment