Mwenyekiti
wa taasisi ya Policy forum Gotfried
Sangana akiwasilisha mada ya utawala bora wakati wa mijadara hiyo mapema leo
katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Da Es Salaam.
|
Watoa
mada katika mdaharo huo, kutoka kushoto ni Dr. Ryoba katikati Prof. Easter
Dungumero kutoka Chuo kikuu cha Dar Es Salaam na mwisho Prof. Joseph Semboja wa
Taasisi ya Uongozi nchini.
|
Wadau wa mdahalo kutoka ofisi ya Rais sekretarieti ya utumishi wa umma kulia ni ndg Kipacha na mwenzake kutoka ofisi hiyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mapema |
HABARI KWA UNDANI:
Mdahalo
wa taasisi za serikali, dini na asasi za kirahia umefanyika katika hatua ya
kutaka jamii na taifa kwa ujumla kurejea kwenye mfumo wa maisha unaojali na
kuthamini maadili pasipo kuweka mbele ubinafsi.
Maadili
ni moja ya hatua muhimu sana na ambayo humtambulisha mtu katika jamii yake na
katika hali ya kawaida maadili hujitokeza katika matendo ya maana ndicho
kielelezo sahihi cha kupima maadili ya sehemu au jamii.
Ikiwa
ni mdahalo wa pili kufanyika kitaifa katika kuadhimisha siku ya maadili na haki
za binadamu mnamo Desemba 10 2016, kampeni ya taifa ya kujenga na kukuza
maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya
rushwa inafanyika katika kujenga utamaduni wenye maadili mema kwa kizazi cah
sasa na kizazi kijacho.
Akifungua
mdahalo huo, waziri wan chi Ofisi ya Rais menejiment ya Utumishi wa Umma na
utawala bora Mh. Angela Kairuki amesema, katika kuunga mkono jitihada za
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuri, kauli mbiu “Kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu,
uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa inapewa nafasi katika
maadhimisho hayo, amesisitiza siyo siri kuwa
kadiri siku zinavyosonga mbele suala la maadili ni changamoto siyo kwa Tanzania
bali hata kwa duniani kwa ujumla,
vitendo vya rushwa, ufisadi na ukiukwaji wa haki za biandamu vimeendelea kuwa
ni tatizo la dunia nzima.”
Hata
hivyo amegusia jinsi matendo ya unyanyasaji kutokana na mauaji ya kutisha
yanayofanywa kwa walemavu na ngozi (Albinism) kuwa kiasi kikubwa inachangiwa na
ukiukwaji wa maadili. Pamoja na hilo vyombo vya dola vyenyewe haviwezi kumaliza
tatizo hili na mengine,” jamii nzima ipinge na
kutokomeza vitendo vyote vikiwemo vya ufisadi, rushwa, ukiukwaji wa maadili na
haki za binadamu ili kuliletea taifa letu maendeleo.”
Naye
Jaji mstaafu Amily Ramadhani Manento anasema; pamoja na suala la maadili kuwa
pana sana lakini “maadili yanaanzia juu kwa
viongozi wa juu, maana viongozi wa juu wakiwa na maadili basi watayashusha
chini, mfano hapa nchini kuna utawala ulioachwa, utawala wa maandishi, maana
unakuta kuna mmoja kakosea ni vizuri ukamuandikia, na unapomwandikia unamueleza
alipokosea na yeye anajieleza ili uweze kumpima wakati unapomtathimini katika
nafasi yake ya uongozi.”
Jaji
manento ameelezea kuwa unapomwandikia na kuwa siri au katika muktadha wa onyo
basi mwajiliwa huyo anakuja kuwa mtumishi mzuri kwatika uongozi, lakini “tabia iliyozuka hivi karibuni ya kulindana na kusema
usimchafulie mwenzako faili lake, unamuita na kumueleza na akitoka hapo
anaendelea na mambo yale yale, hivyo basi utawala wa mawasiliano (administration
by correspondence) unapunguza tatizo hilo”.
Akijibu
swali la mwanahabari juu ya utumbuaji majipu unaofanywa na viongozi wa serikali
kwa kipindi hiki anasema “kiongozi wa chini huwezi ukamjadili kiongozi wako wa
juu hadharani, nikiwa chini ya mheshimiwa Rais maana hiyo inakuwa ni sawa na
kukosa adabu, lakini mkuu wa wilaya na mkoa anayefanya hivyo ni kutokana na
maelekezo ya Mh. Rais."
Post a Comment