0

Tanzania inasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa wa wanyamapori barani Afrika na duniani kote, ikiwa ni nchi ya pili kuwa na rasilimali nyingi asili na iliyotenga sehemu kubwa ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi (24%) ili kuhakikisha kuwa wanyamapori na ndege wapo salama na wanalindwa.


Twaha Twaibu Afisa mkuu wa wanyamapoli wa wizara ya Maliasili na Utalii nchini, akitoa maelezo wakati wa kongamano la kampeni ya kulinda maliasili za taifa, jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa -AICC.


Siraha na risasi kama hizi zimekuwa zikitumika kuangamiza wanyama walio katika hifadhi zetu.

Hivi siyo vipande vya miti fulani kama mianzi, ni pembe za tembo ambazo mara baada ya Tembo wetu kuuwawa uonekana hivyo.


Pamoja na juhudi nyingi za kuzuia uharifu huu wa kusikitisha kwa Tembo wetu, hali kama hii inapaswa kupingwa na ushiriki wa kila mwananchi
Pamoja na juhudi  nyingi zinazofanywa, uvamizi wa mifugo, ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo bado imeendelea kuwa changamoto kubwa ya kiuhifadhi hali inayopelekea na kuathiri siyo tu kuuawa kwa wanyamapori, bali pia inahatarisha utalii pamoja na usalama wa nchi yetu. 

Pamoja na ujangili, mapito/njia au shoroba za wanyamapori zinaendelea kuzibwa na uvamizi wa mifugo ya wafugaji, shughuli za binadamu katika maeneo yaliyohifadhiwa.

Hali hii inasababisha kuongezeka kwa migogoro baina ya wanyamapoli na binadamu hali inayopelekea kupungua kwa idadi ya wanyamapori hususani tembo ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.

Dkt John Pombe  Magufuli rais anayeongoza serikali ya awamu ya tano inayoendelea kukabiliana na ujangili kwa nguvu zote kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutekeleza mkakati wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara za serikali iliyozinduliwa Novemba 2014 Arusha (National Ant poaching Strategy to Combat Poaching and Illegal Wildlife Trade)

 Doria  na intelijensia ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa zinaendelea kufanyika nchi nzima. Hii inakwenda sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu uhifadhi wa maliasili.

Post a Comment

 
Top