Jani la mmea wa Bangi ambao unatumika kama dawa za kulevya nk. |
Leonard Mutani -Arumeru
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Katika matokeo ya mtihani
wa elimu ya sekondari nchini, shule iliyochukua nafasi ya juu nchini imetokea
katika mkoa wa Arusha wilaya ya Arumeru ikiwa inapatikana katika kijiji
kinachojulikana kama Kisimiri ambalo ndilo jina la shule hiyo iliyopo katika
kitongoji cha karafia.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa na mtuhumiwa aliyekamatwa na magunia mawili ya bangi katika kijiji cha Kisimiri Wilayani Arumeru. |
Mkono mmoja hauvunji kijiti, Ushirikiano uzaa matunda, kama ambavyo askari hawa wa wanyama poli wakisaidia kushusha na kupakia magunia zaidi ya bangi. |
HABARI KWA UNDANI:
Mara kadhaa eneo hilo
wananchi wake wamekuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza mazao ya nyanya
ambazo ndiyo zao kubwa la biashara na limewapatia fedha zilizopelekea
kubadirisha maisha yao, hivyo basi wananchi wengi wamejikita katika kilimo cha
aina hiyo ambayo inapandwa na kufikia hatua ya kuvunwa kwa muda wa miezi
mitatu.
Inasemekana ukulima wa
bangi ulianza tokea wakati mkoloni katika eneo hilo, hivyo hakuweza kuacha aina
yoyote ya mazao iwe ya chakula au biashara yaliyoweza kulimwa ili kuwanufaisha
wananchi hali hiyo inapelekea wananchi kufanya kilimo cha bangi inayostawi na
kusemwa ni bangi nzuri kutokana na kumea eneo lenye hali ya hewa yenye baridi,
hivyo imefanya kijiji hicho kuwa korofi kwa ukulima wa zao hilo linalopigwa
marufuku nchini.
Mnamo October 10.2016
mkuu wa wilaya ya arumeru Alexandra Mnyeti alifanya mikutano kadhaa katika
maeneo yanayosemekana kukithiri kwa kilimo na biashara ya bangi ambapo katika
mikutano hiyo na viongozi wakiwemo mkurugenzi, madiwani, watendaji, wajumbe na wenyeviti
wa vijiji ambapo alitoa maagizo kwa wananchi kumtaja mtu yeyote anayefanya
biashara au kulima zao hilo.
Kufuatia tamko hilo la
mkuu wa wilaya, wanakijiji wa kisimiri chini wameshirikiana na viongozi wao na
kupelekea kukamatwa kwa zaidi ya magunia thelathini na mbili (32) ikiwemo mbegu
ya bangi debe nne (4) inayokisiwa kuweza kupandwa kwenye shamba lenye ukubwa wa
ekari 60, hali inafanya kuweka historia ambayo haijawahi kutokea ya kumatwa kwa
mbegu nyingi kiasi hicho huku mmoja wa watuhumiwa ajulikanaye kwa jina la
Emmanuel Ndereko akikamatwa na magunia mawili.
“Sehemu
nyingine nchini imekuwa ikitumika nguvu kubwa kumamata bangi, lakini katika
eneo hili matunda ya mkuu wa wilaya ya kukaa na viongozi walio chini yake
yamefanya hata jeshi la polisi kuwa na kazi ndogo hata ya kukamata wanaohusika
na biashara hii.” Anasema mkurugenzi wa wilaya
ya arumeru Christopher J. Kazari.
Kutokana na kupakana na
nchi jirani ya kenya na umbali mfupi kutoka vijiji jirani vinavyolima zao hilo,
usafirishaji wake umekuwa ni mwepesi huku pikipiki, magari hata wanyama kama
punda ambao wamefundishwa kubeba magunia ya bangi na kupeleka kuvuka mpaka kwa
njia za panya na kupeleka sehemu husika pasipo kuongozwa na mtu, alieleza afisa
utalii wilaya ya Meru.
Hata hivyo katika
kuhakikisha zao hili halilimwi na kuuzwa katika eneo hilo, mkurugenzi wa wilaya
ya arumeru anahainisha mikakati ambayo inawagusa watendaji wote ikiwa ni kila
mtu na nafasi yake kufanikisha zoezi hili, pia wakaazi wa maeneo husika ili
kujua ni aina gani ya mazao ya mbadala yanawezwa kulimwa zaidi ya bangi, hivyo
wataalam wa kilimo wataletwa kupima ni na kushawishi aina mazao yanayofaa.
Post a Comment