0

Makao makuu ya kanisa la Roman katoliki duniani Vatican 

Dunia ikiwa inazidi kuwa sehemu ndogo kutokana na mawasilino, teknolojia kuwa pana na kila mtu aliye kwenye mazingira mazuri ya kufuatilia kila jambo awe wa dini au asiye na dini wanatafuta taarifa kila sehemu inapopatikana.



Jiji la Vatican ni makao makuu ya kanisa la Roman katoriki duniani, sehemu ambayo ndipo yalipo makazi ya kiongozi huyo wa juu kabisa wa kanisa hilo lenye historia ndefu kutokana na mapitio yake yanayogusa watu waliomo katika uso wa dunia. Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni ikiwa ni mara ya kwanza kwa kanisa hilo iliyoonyesha tabia na mienendo na nidhamu ya viongozi wake.


Askofu mkuu Silvano Tomasi ambaye ni balozi wa umoja wa mataifa huko Geneva.

Askofu mkuu ambaye pia ni balozi mjini Geneva kwa umoja wa mataifa Silvano Tomaso amebaini takwimu hizo wakati wa mkutano wa kutafuta njia za utekelezaji wa mikataba ya umoja wa mataifa dhidi ya mateso, ambapo alisisitiza jinsi mikataba hiyo inavyotumika kidogo katika mji wa Vatican.


Hata hivyo alitoa takwimu jinsi gani sehemu hiyo inavyotoa hukumu kwa kesi za ngono zinazohusu unyanyasaji kimataifa, na katika hatua nyingine hakuweza kubishi wakati wa mkutano huo kwamba unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto ilichukuliwa katika mateso. Askofu aliendelea kusema, tangu mwaka 2004 zaidi ya kesi 3400 zinazo aminika kuwa za matumizi mabaya ndani ya mji wa Vatican ikiwa ni pamoja kesi 401 kwa mwaka 2014.

Askofu Tomaso anasema katika muongo uliopita makuhani wapatao 848 waliondolewa  au baadaye kurudishwa kwenye nafasi zao kutokana na nafasi ya papa, pia ilitokea wengine 2572 kuhukumiwa maisha kwa toba na maombi huku wengine kati yao wakipata adhabu nyingine ndogo ambazo hutumika pale inapoonekana kuhani muhusika umri wake umekwenda na anaonekana ni mzee au mgonjwa.

Hata hivyo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa; “hakuna hali mbaya ya hewa yenye kuonyesha ukatili, ila kuna dhamira ya jumla ya kusafisha nyumba, nidhani tunavuka vizingiti, tunavyosema tunapokaribia katika mageuzi yetu, ni wazi kuwa suala la unyanyasaji kijinsia kwa watoto ambalo ni pigo na janga duniani kote, limekuwa likishugulikiwa katika miaka 10 iliyopita na kanisa katika utaratibu mpana kwa njia ya kujenga”

Mkurugenzi wa holy see wa ofisi ya wanahabari Federico Lombardi kulia akimvuta mkono mwanachama wa tume ya kipapa ya pedophilia Marie Collins ili atoke mbele ya waandishi wa habari baada ya kutolewa kwa taarifa ya unyanyasaji wa watoto mjini vatcan.



Post a Comment

 
Top