0

Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM

Chuo kikuu cha Dodoma Udom kikishirikiana na Mamlaka ya chakula na Dawa nchini TFDA wamezindua mfumo wa utoaji wa taarifa unaomwezesha kila mtanzania mwenye kifaa cha kisasa kama simu na komputa ikiwa imeunganishwa na internet kuweza kutoa taarifa.

Prof Aloyce Mvuma wa chuo kikuu cha Dodoma Kitengo cha Tehama anasema mafanikio haya yanakwenda sambasamba kwa watendaji wote waliofanikisha mfumo huu ambao unaleta changamoto kwa watu wote, ikiwa ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa haraka.

Mfumo huu ni umepitia majaribio mbalimbali katika kuufanya ufanikiwe na umetengenezwa na watanzania wazalendo kwa asilimia 100, hatua inayoleta nafasi kupitia mfumo kuwaona na kuwathamini wasomi wataalam wenye uwezo mkubwa kubuni mifumo mbalimbali, katika hilo mikoa 10 ilitumika kufanya majaribio kuona kama utaleta manufaa kwa taifa.


Hata hivyo ameiomba serikali kuwaunga mkono na kuwapa nafasi wasomi wetu pia kutambua vyuo vya elimu ya juu ikiwa na maana kuna watu wana uwezo na hawapewi nafasi, huku chuo kikuu cha Dodoma kinatoa wataalam wa Tehama wenye ujuzi na ustadi.


PICHA: Prof Aloyce Mvuma wa chuo kikuu cha Dodoma Kitengo cha Tehama anasema akizungumzia programu tumishi ya utoaji wa taarifa iliyosanifiwa na chuo hicho kabla ya kuzinduliwa makao makuu ya TFDA jijini Dar Es Salaam.



PICHA: Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiti Sillo akielezea moja karatasi zinazotumika kuchukua taarifa za ubora na madhara yatokanayo na madawa yanayotumiwa na wananchi nchini.




PICHA: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy mwalimu akiteta jambo na Prof Aloyce Mvuma wa chuo kikuu cha Dodoma Kitengo cha Tehama


PICHA: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto aliyesimama akiongea wakati William Reuben -Kaimu mfamasia mkuu wa serikali wa kwanza kushoto, anayefuatia Prof Aloyce Mvuma Udom, Hiti Sillo Mkurugenzi TFDA na Adam Mitangu Fimbo wa mwisho kulia wakimsikiliza waziri.


PICHA: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea kwa kuwapongeza Chuo kikuu cha dodoma na Mamalaka ya chakula na Dawa kwa teknologia hiyo ambayo itakuwa ni msaada kwa jamii, kabla ya kuzindua program tumishi hiyo. 


PICHA: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy mwalimu akielekeza kidole kubonyeza kitufe cha kuzindua rasmi program tumishi makao makuu ya Chakula na Dawa jijini Dar Es Salaam.

PICHA: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Dr. Alex Fabian Nkayamba jinsi program hiyo inavyofanya kazi, mara baada ya kuizindua.


HABARI KWA UNDANI.

majukumu ya TFDA ni kupangilia kutathimini na kufuatililia matumizi ya dawa na vipodozi mbalimbali pamoja na kuhakiki usalama wa chakula, kutokana na hayo fomu maalum kwa ajili ya mteja na watumiaji zitajazwa endapo kutakuwepo na madhara yaliyotokea kutokana na matumizi hayo”  Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiti Sillo anasema.

Fomu hizo zimekua zikisambazwa katika zahanati na vituo vya afya katika maduka yote ya madawa nchini ili ziweze kutolewa taarifa kwa ajili ya kungundua madhara ya dawa kwa haraka lakini utoaji wa ripoti hizo umekuwa ni mdogo ikiwa na maana elimu ya utoaji wa taarifa hizi umekuwa bado haujafikia kiwango kilichowekwa cha taarifa 9,000 kwa mwaka wakati kwa sasa taarifa zitolewazo ni wastani wa 200 mpaka 300 kwa mwaka kulingana na madhara yanayoonekana.

Aitha ndugu Sillo ametoa rai kwa watengenezaji wa madawa kuweka lebo yenye kuashiria madhara kwa matumizi endapo mtu asipofuata maelekezo na utaratibu anaopewa na mtaalam hama daktari, lakini kwa wale ambao hawataweka lebo hatua zitachukuliwa kuanzia viwanda vyao kufutiwa  usajili ili watumiaji wasiweze kupata madhara.

Uamuzi wa kuanzisha na kutumia mfumo huo kwa ajili ya watumiaji kuweza kutoa taarifa mbalimbali,  katika kuangalia ubora na upatikanaji mzuri pamoja na usalama wa madawa pasipo kufika katika ofisi za TFDA bali kwa kupitia simu,laptop ama kwa kupitia website ya TFDA ya www.tfda.go.tz na wao watashulikia taarifa hizo kwa haraka zaidi

Akizindua mfumo huo waziri wa Afya jamii jinsia wazee na watoto  Ummy Mwalimu amesema “mfumo huu unapatikana kwa vifaa vya kisasa ikiwemo simu, komputa, lakini kupitia website ya tfda unaweza kupata taarifa zaidi jinsi ya kuutumia na kuutumia, tfda wanapaswa kushirikiana na sido ili waweze kuwaendeleza wajarisiamali wadogo wadogo  ambao wengi huzalisha bidhaa lakini wanakosa njia za kufikisha taarifa kwa watu wa tfda katika kuhakiki ubora wa bidhaa zao.

Ameomba kitengo cha Tehama cha chuo kikuu cha Dodoma UDOM kuunda program ambayo itamuwezesha mama mjamzito kuweza kugundua maendeleo na kufuatilia njia nzuri kwa mfumo wa kielectroniki.
ni jambo la maana tfda walilogundua kwani matumizi ya simu kwa hivi sasa yameongezeka mno na pia watumiaji wa simu wanapaswa kutumia  katika kujali afya na kutoa taarifa nzuri ama kuripoti taarifa kwa tfda  na sio kuitumia simu katika matumizi yasiyo na misingi yeyote” Amesema Ummy Mwalimu.

Pia anasisitiza utolewaji wa elimu kwa wataalamu wa afya pamoja na elimu kwa jamii ikiwa na kujiwekeza zaidi katika matangazo ili wananchi na watoa huduma  waelewe umuhimu wa mfumo huu, lakini amewataka tfda pindi wanapopokea taarifa mara moja waitolee ufafanuzi pamoja na ufumbuzi na sio kusubiri hadi watu wapate madhara kutokana na  matumizi ndipo waanze kufuatilia zaidi wanapopokea taarifa hata kwa watu kumi basi waweze kuhakikisha wanatatua mapema.

Akijibu swali kuhusu upatikanaji wa dawa bandia mkurugenzi wa tfda anasema; kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mdawa hayo umepungua pamoja na matukio ya wahusika wanaojihusisha, anasema dawa nyingi ni salama. Japo dawa zilizoisha muda wa matumizi anatolea mfano; mtu mmoja mjini musoma alikamatatwa kwenye nyumba ya wageni akiwa na makopo makubwa ya dawa akifanya packing upya kwa dawa zisizo halisi.

Post a Comment

 
Top