PICHA: Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi
nchini Godfrey Simbeye akimkabidhi bendera ya Taifa Asha Abbas mbele ya wanahabari pamoja na wafanyakazi wa ofisi hiyo makao makuu ya TPSF.
|
PICHA: Asha Abbas mshindi wa tuzo ya ANZISHA kwa Tanzania akiongea na kutoa shukurani zake kwa waandaaji wa shindani hilo na kuwaomba vijana wasikate tamaa katika kuanzisha kitu chenye kuleta maendeleo kwa jamii na inapaswa kuwapa moyo ili kufanikisha malengo kwa ajili ya siku za usoni.
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
“mimi ni mwanzilishi wa website ya Aurateen iliyotengenezwa
kwa ajili ya vijana kuuliza maswali online kuhusu afya ya kijinsia na
changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kila siku, wazo hili lilikuja baada ya
kujua vijana wengi wanajihingiza katika mambo mengi yasiyofaa wakiwa katika
umri mdogo wakiwa bado wako mashuleni, pia mivuto kutoka makundi yasiyofaa
yanawafanya kujiingiza katika wizi, madawa ya kulevya, mimba za utotoni, ngono
ktk umri mdogo ambazo ni hatari kwa afya” maneno ya Asha Abbas.
Pamoja na kuelezea hayo
aisha mwenye umri wa miaka 17 anasema wakati akiwa katika jamii aliona ni vema
kuanzisha kitu kinachoweza kuwasadia vijana wenzake waweze kuwa salama kutokana
na changamoto zinazowazunguka.
‘ANZISHA’ ni tuzo
iliyohasisiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ikiwa na lengo la
kumuwezesha mjasiliamali mdogo ambaye ameweza kutekeleza wazo la biashara
alilokuwa anawaza na kulifanya kuwa kitu halisi, ikiwa ni kuleta suluhu ya
changamoto za kijamii, pia kama alianzisha biashara endelevu katika jamii
aliyomo.
Kwa Tanzania TPSF
inashirikiana na chuo kinachowaunganisha viongozi watarajiwa African Leadership
Academy cha Afrika kusini kuitambulisha tuzo hii ya Anzisha Prize Award, ikiwa
ni mara ya pili toka ianzishwe huku Tanzania ikitoa vijana wawili walioshiriki
tuzo hii toka mwaka 2015.
Mkurugenzi mtendaji wa
Taasisi ya Sekta Binafsi Godfrey Simbeye anasema “tuzo
hizi zimekuja kutokana na kuwandaa vijana kuwa viongozi wa Africa na
wajasiliamali na ukiangalia umri ambao wanahitimu kuja kwenye mashindani haya ni
miaka 15-22 ni vijana ambao wapo shule na sisi wengi watoto wetu wapo shule unaweza
kusema ah!, anaanza biashara akiwa na umri mdogo, lakini kuna wanafunzi wa umri
huo ambao tayari wana mawazo ya biashara na mawazo ya kuleta maendeleo”
Katika shindano la
mwaka huu ambalo linatarajia kufanyika nchini Afrika kusuni mwezi huu (Octoba)
linashirikisha mataifa kumi na moja kama Msumbuji, Ghana, Morroco, Madagasca,
Niger, Senegal, Misri, Uganda, Kenya, Ivory cost na Tanzania huku washiriki
wakiwa kumi na wawili wawili kati yao wakitoka kenya, lakini katika washiriki
hao 12 mshiriki toka Tanzania Asha Abbas ndiye mshiriki mdogo kuliko wote.
Wakati shindano hilo
litamtoa mshindi ambaye atapata kitita cha US Dollar 25,000 hata hivyo kila
mshiriki atapata nafasi ya kushiriki mafunzo ya wiki moja ambayo yatapelekea
kufikia mchujo wa kushindanisha wazo ambalo litaonekana kuwa wazo bora katika
mawazo 12 ya washiriki wote kutoka nchi 11.
“tanzania masuala ya ajira ni tatizo, tunatengeneza vijana
kutoka shule na vyuo mbalimbali kila mwaka wanaomaliza ni wengi sana, kuanzia
darasa la saba mpaka chuo kikuu ni vijana wengi sana wanaingia sokoni nakisia
wanafika 1,000,000 sasa tunahitaji tuwe
na mashindano ya ubunifu kama haya watu waweze kujiajili” anasema
mkurugenzi wa TPSF Godfrey Simbeye
Post a Comment