Serikali imeanza
kutafiti matumizi na uunganishaji wa nishati ya umeme kupitia wakala wa nishati
vijijini (REA) ikishirikiana na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) inasemekana
kuwa asilimia 10 ya watanzania waishio mijini ndiyo walikuwa na nishati ya
umeme pale serikali ilipoanzisha taasisi ya takwimu huku asilimia 2 ya watanzania waishio
vijijini ndiyo walikuwa na uwezo wa kupata huduma ya umeme, lakini kutokana na
jitihada na utafiti inaonyesha mpaka muda huu ni asilimia 52 ya watanzania ndiyo
walio na nishati ya umeme.
PICHA: Mkurugenzi wa Takwimu na Sera za Jamii Ephraimu Kwesigabo aliyenyoosha kidole akizungumza, kulia kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa REA nchini Eng. Gissima Nyamo-hanga. |
PICHA: Kushoto ni Titus Mwisomba meneja wa NBS na Kulia kwake ni Pius Kasikana pia NBS, wakimsiliza mkurugenzi wa sera na Takwimu za Jamii hayupo pichani. |
HABARI KWA UNDANI
Kaimu mkurugenzi mkuu
wa REA nchini Eng. Gisima Nyamo-hanga anasema utafiti huu utahusisha jumla ya
maeneo ya vijijini na mijini yaliyochaguliwa kitaalam 676 katika mikoa yote ya Tanzania
Bara huku ikihusisha jumla ya familia binafsi 10,140 ikiwa ni pamoja na
viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusiana na miradi mbalimbali
ya maendeleo katika maeneo yao.
Katika kipindi
tulichopo kwa sasa dunia imejikita kwenye sayansi na teknolojia hivyo utafiti
huu wa kuwangalia hali ya upatikanaji wa nishati nchini utaelekea katika njia
hiyo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki na wadadisi watatumia simu za kiganjani
kuwahoji wanafamilia na viongozi wa vijiji pamoja na mitaa baadaye kujaza
majibu ya mahojiano hayo kwenye madodoso yaliyopo kwenye simu zao.
Utafiti huu ni wa
kwanza kufanika kwa kuhusisha mikoa yote ya Tanzania Bara, hivyo upatikanaji wa
takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa zihusuzo hali ya upatikanaji na
usambazaji wa nishati ikiwa ni pamoja na takwimu zake kutumika kuendeleza
mipango ua usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali.
Hata hivyo ametoa
tahadhari kutokana na yale yaliyotokea mkoani Arusha kwa kuuwawa kwa watafiti watatu, “nawaomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwadhuru
wadadisi watakapokuwa katika majukumu yao kwa ajili ya kuisaidia nchi, mtu
yeyote atakayepatikana na hatia ya kuwazuia kutekeleza kajukumu yao
atachukuliwa hatua kwa mujibu wa shera ya Takwimu kifungu cha 37 ya mwaka 2015”
alisema.
Post a Comment