0


Na Timothy Marko
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuri imeweka msisitizo mkubwa  juu ya kujenga uchumi wa viwanda, Tanzania pamoja na serikali ya China wamefanya makubaliano yanayofikia shilingi bilioni 97 ili kuweza kuinua sekta ya viwanda kupitia mikoa ya ukanda wa pwani.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda kutoka nchini China pamoja na Tanzania jijini  Dar es salaam waziri wa viwanda na Biashara Charles Mwijage amesema, fedha hizo zitajumuisha kufanya maboresho ya ujenzi wa bandari ya bagamoyo na kuweza kuboresha miundo mbinu  ya reli ya kati sambamba na uboleshwaji wa bandari ya Zanzibar.

PHOTO:   Naibu waziri wa Biashara wa China kulia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania Mh, Charles Mwijage kushoto.

 “Hali ya ukuaji wa uchumi inaenda sambamba na ukuwaji wa sekta ya viwanda ili, kuiwezesha nchi ya Tanzania kufikia malengo yake ya nchi ya uchumi wa kati, sekta ya viwanda hainabudi kuwekewa mkazo, hivyo serikali  kwa kulitambua hilo kwa mwaka huu na mwaka ujao imelenga kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kupitia sekta ya viwanda” Alisema waziri wa  viwanda na biashara Charles Mwijage.

Hata hivyo waziri Mwijage amesema; katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda imelenga kutumia fedha hizo katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha vigae katika wilaya mkuranga ambacho kinaendelea kujengwa wakati jumla ya dola milioni 150 zinatarajiwa kutumika kukamilisha kiwanda hicho.

Sambamba na ujenzi wa kiwanda hicho mkoani pwani, serikali kwa kushirikiana na nchi ya China inatarajia kujenga viwanda vya nguo chenye urefu wa kilometa za mraba 2,400.

"tutandelea kukuza uhusiano wetu kati yetu na nchi ya china kwani uhusiano wetu na china niwakitambo kirefu tangu enzi za uhuru amekuwa rafiki wakaribu sana na Tanzania, hivi karibuni china inatarajia kuanzisha maonesho ya kibiashara nchini china, Tanzania tumepata mwaliko katika maonesho hayo’’ Aliongeza Waziri Charles Mwijage.

Aidha kwa upande wake Naibu waziri wa Biashara wanchini china Quan Keming amesema kutokana naTanzania kuwa na ukuaji wa uchumi wa kasi ikiwemo uboreshwaji wa miundo mbinu nakuweza kufikia dira ya maendeleo 2025 china itaendelea kuisaidia Tanzania imekuwa ni nchi rafiki kwa muda mrefu.





English story: 

China, Tanzania sign  97/- bil for docks rehabilitation

CHINA and Tanzania signed memorandum of understanding for national rehabilitation of all docks with inclusion of Dar es Salaam and Zanzibar and
bagamoyo construction worth of 97 /-billion.

The Ministers for Trade and Industry Tanzania Charles Mwijage and China’s Deputy Minister Quan Keming jointly signed it at the Ministry of Finance in Dar Es Salaam yesterday.

 The Minister Mwijage highlighted before the business stakeholders from both countries that the funds would be utilized accordingly for national economic development.

However he said the Central corridor rail will not be left behind as well since it’s also on the   forefront for national development plan.

Besides, Mwijage briefly said about USD150 m will be used to construct tiles factory at Mkuranga that is an on going in Coastline district. Soon China is expected to build textile manufacturing industry of 2,400 Km in the same district.

Quan Keming said the China’s Government will keep on assisting the Government of the United Republic of Tanzania for economic and social development. China does help this Government as its intention is to be fully industrialized for its people’s enjoyment.


Post a Comment

 
Top