0
Leonard Mutani.
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM

Hizi ni baadhi ya picha chache ambapo kama ulikuwa hujui ndicho Chuo kikuu cha Muhimbili cha Sayansi na Tiba ambacho kinakuja kuwa chuo kikuu kikubwa katika ukanda huu wa Afrika mashariki, chuo hiki kipo nje kidogo ya jiji ;la Dar Es Salaam katika eneo la Mloganzira wilaya mpya ya Ubungo km zaidi ya 20 kutoka katikati ya jiji.


PICHA: Hapa ni upande wa mbele ukiwa unaingia kuelekea lango kuu la kushuka kuingia ndani ya jengo hilo lenye olofa zaidi ya kumi na upande wa chini ya aridhi likiwa na sehemu nyingine.

PICHA: Kwa sababu ni chuo cha tiba na matibabu yatakayokuwa yanatolewa hapo hapo basi umeme ni masaa ishirini na nne hata ukikatika kuna haya majenereta yapo standby kwa dharula yoyote. 



PICHA: Mara kadhaa umekuwa ukitembelea hotel na sehemu maalum nzuri ambazo mazingira yake yanakupeleka katika mawazo kuja kuishi au kufikia hatua ya kuishi hapo, picha hii inaonyesha sehemu ya mbele ya baada ya kutoka kwenye gari kabla ya kuingia ndani ya jengo la chuo, ndivyo inavyoonekana.

PICHA: Sehemu mbali mbali ikiwa ni hotelini, viwanjani na hata hospitalini kumekuwa hakuna sehemu maalum ambayo kunaonyesha alama kama hizi, ukiona sehemu yoyote kuna alama kama hii basi tambua ni maalum kwa mlemavu. Katika chuo kikuu cha MUHAS Mloganzira sehemu ya kuegeshea magari kuna alama hizi ikionyesha ni sehemu maalum kwa ajili ya walemavu.


PICHA: Huu ni upande wa nyuma wa chuo hiki ambacho kwa taarifa nyingine baadhi ya wanachuo wanaokuja hapa tayari wanaonyesha hamu ya kuja kujifunza na kupata elimu hapa kutokana na mazingira yake yanayovutia.

PICHA: Bustani hii hipo upande wa nyuma wa jengo kuu, hapa ni mwanzo tu ambapo nyasi ndiyo zimepandwa, kwa mbali kama vibanda ni sehemu maalum za kupumzika zikiwa zinazungukwa na maua mbalimbali.

PICHA: Dar Es Salaam linafahamika kama jiji lenye joto sana, hata kufikia nyuzi joto 32, lakini katika chuo hiki kimefungwa mfumo wa kupata hewa nzuri na hii ni mitambo iliyopo chuoni hapo hapo ambapo ikiwashwa kila chumba na kolido kitapata hewa safi kutokea hapa.
PICHA: Hapa ni sehemu ndogo tu ya vitanda maalum kwa wajili ya wagonjwa na utafiti kwa magonjwa mbalimbali yatakayokuwa yanafanyiwa utafiti, inasemekana baada ya chuo hiki kufunguliwa hakutakuwa na haja kwa baadhi ya wagonjwa kusafilishwa kwenda nje kutokana huduma za matibabu zitakazokuwa zinatolewa hapa.




Post a Comment

 
Top