0

PICHA: Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe mwenye kaunda suti nyeusi akiongea na baadhi ya wanachuo Theodora Salastian kiwaly kulia na Sonia Twalipo Mwakipesile kushoto alipofanya ziara chuoni hapo.

PICHA: Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe akisikiliza jambo kutoka kwa msaidizi wa maktaba Edwin Kilawe mwenye shati jeusi kulia alipoingia maktaba kujiridhisha.

PICHA: Wafanyakazi, walimu na watumishi wa wizara ya Maliasili na Utalii kitengo cha chuo cha taifa cha utalii wakimsikiliza Prof. Jumanne Magembe alipokuwa anazungumza nao juu ya mambo kadhaa katika ukumbi wa chuo hicho.




HABARI KWA UNDANI:

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe.
Leonard Mutani TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM

Waziri wa maliasili na Utalii nchini Prof. Jumanne Magembe amewataka watendaji wa chuo cha utalii cha Taifa kuweza kukiendesha kwa faida na kutokutegemea ruzuku kutoka serikali kuu.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea moja ya idara anazozisimamia katika wizara yake Prof. Magembe amesema, ni vema chuo hicho kiweze kuboresha mitaala yake ikiwa ni pamoja na kuendana soko la utalii nchini, kwani sekta hiyo imekuwa ni kitovu kikubwa cha uchumi na mapato kwa taifa.

ninataka mboreshe mitaala yenu, ili kuendana na soko la utalii, wanafunzi watakaofundishwa hapa waweze kuajiliwa sehemu yoyote nchini na nje ya nchi hususani katika hoteli zenye ngazi ya nyota tatu hadi tano popote duniani” alisema Prof. Magembe.

Hata hivyo Prof. Magembe amesema kuwa ni ajabu kuona baadhi ya hoteli nchini zenye nyota tano zikiwa hazina wafanyakazi wazalendo wa kitanzania badala yake wanachukua wafanyakazi kutoka nje ya nchi, pia amesikitishwa na kitendo cha chuo hicho kutokuwa na mazingira yasiyoridhisha ingawa wana kila kitu kinachotakiwa kufanyika kuwa cha kisasa.

Aidha waziri Magembe ameshangazwa na kitendo cha bodi hiyo kutothamini sekta ya utalii ambayo imeonekana kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 500,000 huku walio nje na walio jiajili wenyewe kuwadumia watalii ni 1,200,000 hata hivyo amesisitiza kuwa sekta hiyo kiini chake kipo kwenye katika sekta binafsi.

Katika hatua nyingine Waziri Magembe amewataadhalisha watendaji wa chuo hicho kujitathimini kwa kutoigemea serikali kwa kuililia kupewa ruzuku na kuwafananisha sawa na machungwa yaliyowekwa mahala pasipokuwa pake.

Anasema, “wakati tunaanza kujenga chuo hiki, tulichimba msingi mimi na waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa ufaransa wakati huo nilipata bahati ya kuwa waziri wa maliasili na utalii, lakini malengo yetu yalijikita kwenye eneo moja kwamba tutafundisha wataalam wenye ujunzi, wataalam wa sekta ya utalii.”


Wakati huohuo amewataka watendaji hao kutobadiri malengo ya chuo hicho kutoka kutoa wataalam na waache mara moja kujifanya kuwa mawakala wa sekta ya utalii na mahoteli nchini. “Kuanzia sasa hiki chuo siyo wakala ni chuo cha Utalii cha Taifa.” Alisema Prof Magembe.

Post a Comment

 
Top