0
PICHA: Balozi wa umoja wa ulaya nchini Roeland Van de Gear akiongea juu ya maadhimisho ya utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani, mapema leo katika ofisi za British Council.





Haki ya kuishi ndiyo haki ya msingi kabisa kwa binadamu ambayo haki nyingine zote zinategemea uwepo wake, kwa hiyo ni lazima ilindwe. Adhabu ya hii  ni kielelezo chenye ukweli kinachohakisi ukiukwaji wa haki za binadamu za kuishi.

Mwaka 1886 ndiyo mwaka ambao kwa mara ya kwanza hukumu ya kifo ilifanyika chini ya serikali ya kikoloni ya kijerumani, baaada ya wakati huo kumekuwa na watu wa haki za biandamu duniani ambao wamekuwa wakipinga adhabu ya kifo ikiwa na maana ya kuiondoa katika jamii kupitia serikali zinazotekeleza tukio hili ambayo siku maalum ya tukio hili ni 10.10  ya kila mwaka.

Haki ya kuishi kwa raia yeyote inalindwa na kikatiba chini ya ibara ya 14 ya kikatiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ambapo ulinzi huu unatolewa kikatiba si ulinzi kamili/halisi, pamoja na hilo nchini Tanzania inasemekana miaka 20 imepita pasipo hukumu ya kifo kutekelezwa.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ofisi za British Council jijini Dar Es Salaam na kuudhuliwa na Balozi wa umoja wa ulaya, Balozi wa Itaria, Sweden wakiwemo viongozi wa kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yamefanyika ikiwa na nia ya kuitaka serikali kuondoa hukumu hiyo ya kifo.



PICHA: Ndugu Mahame Nyanduga 
Pamoja na hayo Mahame Nyaduga ambaye anasema baadhi ya nchi afrika zimefuta sheria hiyo ya kifo kama Guinea, Djibouti, Afrika kusini, Senegal, Rwanda, Congo Brazzaville na nyingine kadhaa zilizo ulaya. Pamoja na hilo nchini Marekani hutekelezaji wa hukumu ya kifo umekuwa ukifanyika kwa njia mbalimbali na nyine zisizo za kimhakama.

Aidha aliongeza kwa kusema; adhabu ya kifo aisaidii kutoa mafunzo au kutubu kwa mkosaji bali kinachofanyika ni utesaji na kumuondolea uhai, na inaifanya serikali isiweze kukwepa kigezo cha mauaji maana imehusikakatika utekelezaji wa kifo. “kisaikolojia mtu aliyehukumiwa kifo hajui hatma yake”

Mjumbe wa balaza kuu la urama kutoka  BAKWATA Ally Khamis, anasema mwaka 610AD ni mwaka ambao Quran ilishushwa, hivyo sheria hiyo haijulikani ilikuja lini, japo kwenye Quran sura 2 iitwayo surat bakara haya ya 178-179 inaeleza vema kuhusu hukumu hii.

Vinginevyo anasema “kumyima mtu haki yake ni kosa na aliyeuliwa naye anapaswa kutetewa maana aliyemuua ana haki ya kuuwawa kwa kutenda kosa la kuua, mfano; gaidi anakuja kutekeleza tukio la mauaji kwa bomu, alafu sheria inasema ahurumiwe au aachwe, hapo haiwezekani naye ni muuaji anapaswa kupata haki yake, suruhu ni bora kuliko kufuata sheraia” alisema.


Wanasheria mbalimbali waliohudhulia maadhimisho hayo akiwemo  mwendesha mashitaka Neema Haule anasema nia ya sheria hiyo siyo tu kutekeleza hukumu ya kifo bali ni katika kutekeleza sheria ikiwa ni kuangalia jinsi gani hata muuaji anaweza kutetewa kutokana na kitendo hicho, ikiwa na maana kuna uwepo wa sheria si sababu ya kuacha kushugulikia haki kama kesi imeletwa mahakamani ili haki iweze kupatikana.

Post a Comment

 
Top