PICHA: Aina ya majengo ya hospitali ya mama na mtoto yanayotarajiwa kujengwa mkoani Arusha. |
Taarifa kamili na Nanyaro Ephata -Arusha.
Maternity Africa waliingia makubaliano na ARDF pamoja na Mawala trust kujenga hospitali ya mama na mtoto.
Ardf walitoa wazo na Mawala alitoa kiwanja na maternity africa wametoa gharama za ujenzi, vifaa vya hospitali pamoja na uendeshaji.
Hivyo ARDF ndio mlinzi wa ardhi waliyoipata kutoka kwa Mawala na kisha kumpa Maternity Africa ili kutimiza lengo/ahadi. Hivyo basi Mkuu wa mkoa alialikwa na Maternity Africa kuja kuzindua mradi huo.
Hata hivyo ligoma kuja kwa kisingizio kuwa hataki Mbunge Godbless Lema azungumze na asiwepo. Akadai pia kiwanja hicho amesikia ni cha mke wa Mbunge Neema.
Wille Mawala katika kikao hicho ameshangaa mkuu wa mkoa amepata wapi habari hizo wakati Nyaraka zilizopo ambazo amemuonyesha kuwa ni kiwanja cha ARDF kwa ushirika na Mawala Trust.
Zimefanyika hatua za makusudi kwa ngazi za juu Mkuu wa mkoa amethibitisha anakuja na hata hivyo asipokuja ratiba ya Uzinduzi na ujenzi itaendelea kama kawaida.
Post a Comment