Rais mstaafu wa awamu
ya tatu Benjamin Mkapa akinyanyua baadhi ya dvd/filamu juu moja kwa moja
kuziweka sokoni kwa wageni waalikwa kununua na kuangalia mambo malimmbali ya
utalii yaliyomo.
|
Kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, father Godwin Rugambwa, Prof. Wenaslaus Kilama na Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua filamu ya karibu Bwanjai. |
Prof. Kilama akimkabidhi Rais mstaafu Mkapa baadhi ya kalenda kwa ajili ya kumbukumbu zikiwa na picha mbalimbali za maeneo ya kitalii kutoka bwanjai, kushoto anayeangalia na father Godwin Rugambwa. |
HABARI KWA UNDANI:
Historia ni sehemu moja
ya kuelezea na kusimulia kile ambacho kilifanyika au kuwepo wakati fulani kwa
wale ambao hawakuwepo hama kupata kuwepo wakati huo.
Katika uzinduzi wa filamu/dvd
inayoonyesha mvuto kwa utalii na yanayoelezwa na Geofrey Meena wa bodi ya
Utalii nchini kuwa atayapeleka katika bodi ili eneo hilo liingie na kuwa moja
ya kivutio cha utalii nchini.
Profesa Wenaslaus
Kilama mmoja wa wasomi waliotumikia taifa miaka ya nyuma ambaye baada ya
kustaafu aliamua kwenda kuishi Kagera ili kutimiza njozi aliyokuwa nayo iliyopelekea
kutengeneza filamu inayoonyesha utalii wa mambo mbalimbali yaliyopo katika eneo
la Bwanjai lililopo wilaya ya Misenye mkoani kagera.
Bwanjai ina mvuto
kutokana na mazingira na utalii wa aina mbalimbali kama; maua, wanyama, ndege,
nyoka na wadudu wa kila aina huku kukiwa na eneo linalosemekana kushabiina kimazingira
na eneo moja lililoko nchini Ufaransa.
Prof. Kilana anasema; “tunapojenga hostel
tuanataka watu wanaokuja Bwanjai waulize kuna nini eneo hili?, kutokana na
swali hilo ndipo wataonyeshwa filamu hiyo ndipo nao watasema hebu mtupeleke
tukaone kiuhalisia, ndipo tutapata fedha kutoka kwa watalii kwa kulala katika
hosteli nasi kuapata mapato”.
Katika uzinduzi huo
ambao mgeni ramsi alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ambaye
pamoja na kujivunia sehemu hiyo ya utalii, ambayo itasaidia kukuza kipato
kutokana na watalii kutumia magari ya makampuni ya wazalendo, pia aliona upenyo
kwa watalii kuona na sisi ni watu tulio na historian a mazingira yanayopaswa
kuheshimiwa.
Hata hivyo
aliwataadhalisha watanzania kwa kutothamini historia ya kule tulipotoka huku
akisema, “huwezi kujua kwa sasa upo wapi na kwa kutowaeleza wengine dharau
itaendelea kuwepo dhidi ya mtanzania yeyote.”
Post a Comment