BOMA LA KIMASAI LINALOTAMBULIKA KATIKA UTUNZAJI MAZINGIRA. |
Kutoka Arusha:
Moja ya jambo linalofanyiwa mkakati mkubwa katika kuepusha
uharibufu wa mazingira ikiwa ni pamoja na janga la uhuaji wa wanyama kwa njia
haramu -Ujangiri linamkazo mkubwa sana katika jamii.
Kampeni mahususi yenye fursa na inayotoa haki kwa kila Mtanzania
inafanyika jijini Arusha.
HABARI ZAIDI....
Afisa maendeleo manispaa ya Arusha Blandina Nkini akiongea wakati akifungua kampeni ya Cheza, Linda na Uhifadhi katika uwanja wa Sheikh Annri Abeid jijini Arusha. |
Mara baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo wanataasisi wote waliweza kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi. |
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Shirikisho la watu wenye ulemavu nchini SHIVIWATA
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta za Uhifadhi, Utalii na Kupinga
Ujangiri ikiwemo Rafiki Wildlife Foundation ya jijini Arusha wamefanikisha
kampeni maalum yenye lengo la kutoa elimu ihusuyo hatua hizo ambapo mwenyekiti
wa shirikisho hilo Fatuma Ally anatoa ahadi kwa kuweka ushirikiano utakaoweza
kuwa na tija kupitia serikali na sekta za kijamii ili kuweza kutokomeza
ujangili.
Afisa maendeleo ya jamii kutoka manispaa ya jiji la
Arusha Bi. Blandina Nkini ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha katika
ufunguzi wa kampeni hiyo iliyokusanya zaidi ya wadau mbalimbali wakiwemo,
walemavu, Albino na wengineo kutoka mikoa kadhaa nchini alitoa angalizo
kutokana na mkoa kuishiwa wanyama ikiwa ni moja ya taswira inayoonyesha kuuwawa
kwa wanyama kama tembo.
Pia alitoa changamoto kwa wale wanaojiona ni wazima
na kuwadhalau wenye ulemavu kuwa wanaweza kuwa na nafasi na uwezo hata
kuwashinda wao wazima.
Naye Chief Joseph Kulindwa amesema kutokana na
madhara ya kuuwawa kwa wanyama, familia
yenye kutunza na kulinda wanyamapoli na misitu ni familia bora duniani, pia
tusipo kuwa makini tuanweza kujikuta katika mbuga za Arusha tunafyeka na kubakiza
mapoli huku akisisitiza kuwa wawindaji haramu wanatoka mikoa yote ya Tanzania
na si sehemu moja.
Vilevile mwenyekiti wa taasisi ya Rafiki Wildlife Foundation
chini ya mchingaji Matwiga anasema “kila mtanzania ana wajibu wa kulinda maliasili ya nchi kutokana na
katiba na sheria ya nchi inavyosema huku mwenyezi Mungu akiwa ametupatia tunu
hii na katika dunia tukiwa ni nchi ya pili yenye vivutio vya kitalii baada ya
Brazil, lakini kwa ni I tunakuwa nchi masikini, hivyo basi kila mtu ana haki ya
kukemea dhambi ya ujangili ambayo ni sawa na dhambi nyingine.”
Post a Comment