Balozi wa India nchini Sandeep Arya akipeana mkono na Highness Bampenja mmoja wa wachezaji wa timu ya wanawake wakati wa kuwatambulisha na kuwaaga |
Timu
ya wachezaji wanaume ikiwa katika timu ya pamoja na Balozi wa India nchini
Tanzania, wanne kutoka kushoto ni timu kapteni Geophrey Mtawa.
|
< PICHA: Timu mbili za wanaume
na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa mwenye suti kati
waliosimama, wakiwa kwenye bendera ya India ndani ya chuo cha utamaduni cha
India jijini Dar Es Salaam, wa kwanza kulia waliosimama ni Mkurugenzi wa ubalozi
Inder Jit Sagar.
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Katika kukuza
ushirikiano na kuendeleza utamaduni kwa nchi ya India na Tanzania, serikali ya
India kupitia jimbo la Punjab imeandaa ikiwa ni
kwa mara ya sita kombe la Dunia la Kabaddi linalotarajiwa kuanzia rasmi tarehe
3-17.11.2016, ambapo ni mchezo
unaochezwa na timu mbili ambapo kila timu inakuwa na wachezaji saba wanaocheza
uwanjani ikwa akili, nguvu na maarifa ya kuepa inatakiwa mchezaji akiwa
uwanjani.
Mchezo huu wa kabaddi
ni maarafu katika jimbo la Punjab na mikoa mingine ya nchini India ambapo kombe
hilo la dunia litafanyika katika sehemu tofauti kumi na nne katika jimbo hilo,
huku mataifa 13 kutoka sehemu mbalimbali dunia zikitarajiwa kushiriki ambapo kwa
upande wa wanaume ni Marekani, Uingereza, Hispania, Denmark, Iran,
Argentina, Canada, Kenya, Sweden, Australia, Tanzania, Sierra Leone na India
Vilevile kwa upande wa wanawake timu 10
zitashiriki ambazo ni Marekani, Uingereza, Denmark, New Zealand, Mexico, Kenya,
Sierra Leone, Australia, Tanzania na India.
Balozi wa India nchini, Sandeep Arya anasema “Tunafuraha
kwani Timu ya Tanzania itashiriki katika sehemu zote mbili, timu ya Wanawake na
timu ya Wanaume. Wachezaji watakaokwenda India kushiriki kombe la Dunia la
kabaddi kutoka Tanzania ni jumla ya watu 34, pamoja na wanaume 15 na wanawake
13 na makocha 4, mkurugenzi wa timu na viongozi wengine”
Geophrey Edward Mtawa kapteni timu ya wanaume
ansema, “tunaenda kushindana siyo kushiriki tu,
tumejiandaa vizuri baada ya kupata wakufunzi kutoka india ambao wametukubali
japo kambi yetu ilikuwa ni ya muda mfupi lakini tupo vizuri kiujumla”.
Vilevile na Salima Hussein Pontia kapteni wa
timu ya wanawake, anasema “timu ya wanawake ipo vizuri tumefanya mazoezi
ya kutosha, tumejiandaa kisaikorojia kushindana siyo kushiriki kwa hivyo
tunawaahidi watanzania tutarudi na ushindi kwa sababu tumeangalia kupitia
mitandao nchi mbalimbali tunazoenda kushindana nazo tukajipima na kufanya
mazoezi ya kutosha tunaamini tunaweza kurudi na ushindi”.
Safari na maandalizi ya timu hii kuelekea
nchini india imewezeshwa na kudhaminiwa na serikali ya jimbo la Punjab nchini
India, kwa muda wa wiki mbili, wakati timu imekuwa ikifundishwa na kufanya
mazoezi yake katika kituo cha utamaduni wa India kilichopo jijini Dar’ es
salaam ikiwa ni maandalizi ya kombe hilo la dunia.
Hata hivyo Balozi Arya anasema “Tuna imani kuwa
kushiriki kwa timu ya Tanzania katika kombe la Dunia la Kabaddi haitosaidia
kukua tu kwa mchezo wa Kabaddi ila pia uelewano na ushirikiano kati ya watu wa
mataifa haya mawili.”
TODAYS NEWS: Tunazitakia kila la kheri katika mashindano hayo kwa timu zote za wanaume na
wanawake.
Post a Comment