PICHA: Mmoja kati ya panya watafiti wa ugonjwa Kifua Kikuu wanaopatinaka kutoka chuo kikuu cha sua morogoro. |
PICHA: Pius Muhapuli akimruhusu mmoja wa panya wanagundua vimelea vya ugonjwa kifua kikuu (TB) kuanza kunusa kila hatua kwa jinsi alivyoelekezwa. |
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Wataalam wanaendelea kutafuta njia rasmi itakayoweza kuainisha chembechembe za
zinazosababisha ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) ikiwa ni pamoja na kuzuia kuenea
kwa ugonjwa huo unaoathiri watu wengi duniani.
Microscope, DNA, Hain
Assay nk ni mojawapo ya vifaa vya kisasa vilivyogunduliwa na wataalam wa
ughaibuni kuweza kuchunguza na kupima ugonjwa huo wa kifua kikuu, katika
upimaji kutumia vifaa hivyo bado imeonekana kila kifaa kikitegemea kingine
katika kupata majibu sahihi kutoka kwenye upimaji.
Emmanuel Sichonne ni
mtaalam kutoka NIMR tawi la Mbeya anasema; “toka
nitumie vifaa vya kisasa nimekuwa nikitumia kimoja na kuamia kwenye kingine
maana kila kimoja kinafanya kazi yake na kulingana na teknolojia kukua, ikiwa
natumia Microscope basi baadaye naweza kutumia Genie expert kupata uhakika wa
kipimo katika utafiti wa kifua kikuu”
Wakati teknolojia ya
kisasa ikifanya kazi kuitegemea nyingine kupima na kutafiti ugonjwa, wataalam
kutoka chuo kikuu cha SUA mkoani morogoro, walifanya utafiti kushirikisha wanyama
na wadudu endapo wanaweza kusaidia kugundua aina ya vimelea vyenye ugonjwa wa
kifua kikuu, ndipo walipogundua panya wa
polini (panya buku) wanao uwezo endapo wakipewa mafunzo na kushirikishwa.
Mariam Juma ni mkufunzi
anayefanya utafiti katika kitengo cha Apopo kinachoshugulika na panya chuo
kikuu cha SUA –Morogoro kwa upande wa utafiti w ugonjwa wa kifua kikuu (TB)
anasema; “utafiti huu wa kutumia panya unafaida kubwa
endapo utapewa nafasi katika vituo vya afya nchini maana panya hawa wana uwezo
mkubwa kupima kwa haraka na muda mfupi kuweza kugundua ugonjwa kuliko mashine
za kisasa mfano; wakati mashine inapima watu 20-25 kwa siku, panya hawa
wanapima zaidi ya watu 100”
Pia mkufunzi mwingine
ndg Pius Wildbad Muhafuli anatanabaisha kwanza uvumilivu wa kutoa mafunzo kwa
panya hao toka wanapokuwa wadogo mpaka kufikia miaka anayotakia kuanza
kuchunguza ugonjwa kuwa ni kipindi ambacho kinataka uvumilivu wa hali ya juu
kutokana na kufanya kazi na kiumbe kisicho na mrejesho kwa kile
unachomfundisha.
Pamoja na mambo mengi
yanayohusu panya hao anasema; “wakati majibu yanayotoka
baada ya kupima TB kutoka kwenye cage/bar yanayopimwa na hawa panya kutopewa
uhakika kwa yenyewe, kwa sasa chuo kikuu cha SUA kipo mbioni kutafiti matokeo
yatakayokuwa ni ya moja kwa moja yasiyotegemea kifaa kingine mara baada ya
kipimo cha panya hawa”
Aitha katika hatua
nyingine ya kuonyesha utafiti huu umeanza kusikika, tayari nchi nyingine za
afrika kama msumbiji walileta wanafunzi ambao tayari walihitimu na kurejea
nchini kwao huku wakiondoka na ‘panya watafiti’ ikiwa ni lengo la kusambaza
utaalam na utafiti.
Katika kuonyesha
utafiti huu kuzaa matunda, chuo kikuu cha sua kupitia
kitengo cha Apopo kinachohusika na panya kikishirikiana na wenzao wa msumbiji kilipata
Tuzo/Award katika mji wa Dubai falme za kiarabu.
Mkufunzi Pius pamoja na
Mariam wanatoa wito wautambue utafiti huu wa panya ambao duniani ni wa kwanza
na umehasisiwa hapa Tanzania na watanzania pia anawasihi wananchi kujitokeza
kwa wingi kupima ugonjwa wa Kifua kikuu ambao unaambukizwa kwa njia ya hewa na
kwa haraka sana, kwenda kuchukuliwa sampuli ambazo wao uzichukua na kwenda
kufanyia utafiti.
Post a Comment